• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

barabara ya Bigwa Kisaki sasa kuanza kujengwa

Posted on: February 12th, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameaahidi kuanza ujenzi wa Barabara ya kutoka Bigwa hadi Kisaki Mkoani Morogoro kwa kiwango cha lami kwa kuwa ombi la kujenga barabara hiyo limetolewa na viongozi wengi na kwa muda mrefu.

Rais Magufuli ametoa aahidi hiyo leo Februari 12, 2021 mara baada ya kuzindua Kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao ya Mikunde cha Mahashree Tanzania  Limited kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Ikiwa siku ya pili ya ziara yake Mkoani humo, Rais Magufuli kabla ya kufungua kiwanda hicho alifungua viwanda viwili  kikiwemo kiwanda cha ngozi na kiwanda cha kukoboa mpunga na hatimae kuzindua kiwanda hicho cha Mahashree Tanzania Limite kilichojengwa kwa ajili ya kuchakata mazao ya jamii ya mikunde.


Amesema, ameamua kulibeba yeye mwenyewe ombi la kujenga barabara hiyo kwa sababu ombi hilo ni la muda mrefu na kwamba barabara hiyo inapitia maeneo muhimu na yenye watu wengi na utajiri Mkubwa, huku akiwataka watendaji wake wa ngazi ya Wizara kuanza kujipanga katika ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu wakianza na  ujenzi wa umbali wa kilometa 40.

Mhe. Rais amefikia hatua hiyo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mhe. Innocent Kalogeresi jana Februari 11 mwaka huu wakati wa siku ya kwanza ya ziara  yake Mkoani Morogoro kwa nyakati tofauti walimuomba Mhe Rais barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami.

Aidha, Mhe. Rais amekubali ombi hilo ya kuahidi ujenzi huo kuanza baada ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mashariki Mhe. Hamisi Tale tale maarufu kama Babu Tale naye kuwasilisha ombi la ujenzi wa barabara hiyo na barabara ya Ngerengere kujengwa kwa kiwango cha lami kwa kuwa wananchi wa jimbo hilo wamekuwa na changamoto ya barabara hiyo kwa muda mrefu..

Awali akiwa katika kiwanda cha MW RICE MILLERS LTD, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kufufua kiwanda cha mafuta cha Moproco kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kisha kutafuta wawekezaji ambao watakiendeleza kiwanda hicho ambacho kimetelekezwa kwa zaidi ya miaka 20.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewataka watanzania wote kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Watendaji wa Mitaa na Watendaji wa Vijiji katika zoezi la kuorodhesha majengo yanayotakiwa kulipiwa kodi kwa Serikali, zoezi ambalo litaanza nchi nzima kuanzia tarehe 15 hadi 28 mwaka huu.

Amesema, lengo la kulipa kodi hiyo kwa serikali ni kupata fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ya nchi na wananchi mmoja mmoja kwa jumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuahidi Mhe. Rais kuendelea kuhamasisha  wawekezaji ndani ya Mkoa na kuendeleza sera ya kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amesema Mkoa huo hadi sasa una jumla ya viwanda 3,652, kati yake viwanda vikubwa ni 25, vya kati ni 16, vidogo 326 na vidogo sana ni viwanda 3285.

Akitoa salamu za Wizara ya Mifugo  na Uvuvi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Olesante Gabriel, amesema Wizara yake kwa sasa wamekomesha suala la wizi wa mifugo hapa nchini hususan  wa ngo’mbe na kwamba wapo katika mkakati wa kupata njia mbadala ya kuwawekea ngo’ombe hao kifaa maalum katika miili yao ambacho kitasaidia kubaini ngo’mbe hao walipo endapo watakuwa wameibiwa.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • RC SANARE ATATUA MGOGORO WA ARDHI.

    April 13, 2021
  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.