• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Hakuna haki bila wajibu

Posted on: March 16th, 2018

Regina Chonjo: Hakuna haki bila wajibu  

Na. Andrew Chimesela -

 Morogoro Baraza la wafanyakazi la Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro limetakiwa kuwa chachu ya wafanyakazi wa Mkoa huo na kuwakumbusha wafanyakazi hao kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili waweze kupewa haki na stahiki zao bila kikwazo pindi wanapolazimika kuzidai haki hizo. Kauli hiyo imetolewa Aprili, 15 mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Regina Chonjo wakati wa kikao cha uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi la Mkoa huo kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa Viongozi wa Baraza hilo.

Mhe. Chonjo amesema, watumishi wa Serikali wanazo changamoto mbalimbali katika utumishi wao ikiwemo nyongeza ya mishahara, posho, madeni, mafunzo, kupanda vyeo na changamoto nyingine, zote hizi ni haki zao za msingi ambazo zitatekelezwa iwapo kuna uwajibikaji kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu, kwa kuwa hakuna haki bila uwajibikaji. “Katika utumishi wetu kuna kitu kinaitwa haki na wajibu, na ili uweze kupata haki ni lazima utekeleze wajibu wako. Lakini vile vile wajibu unaweza usitekelezeke kama yule anayetakiwa afanye wajibu fulani haki yake haioni mbele kama ipo”. Alisema Mhe. Chonjo.” Aidha, Mhe. Chonjo amewataka viongozi na wajumbe wa Baraza hilo kuwa chachu kwa wenzao huku wakijua kuwa kazi yao kubwa ni kuwakumbusha wanaowawakilisha kuwajibika ipasavyo wawapo kazini na kuwa na nidhamu ya kazi huku wakijua kuwa Baraza hilo ni muhimili wa wajibu na haki kwa wafanyakazi wa Mkoa wao.

Naye Katibu wa TUGHE Mkoa wa Morogoro Bi. Sara Rwezaula amesikitishwa na Baraza hilo la wafanyakazi kwa kutofanya vikao vyake ambavyo ni vya kisheria tangu mwaka 2016 na kuwataka Viongozi ngazi ya Mkoa na wa Baraza kubadilika ili baraza hilo liwe na maana kwa Wafanyakazi na kuwaletea tija.

Aidha, Bi. Rwezaula ameuomba uongozi wa Mkoa wa Morogoro kulithamini Baraza hilo ikiwa ni pamoja na kufanyika vikao, ulipaji wa posho kwa wajumbe wake na kutoa mapema taarifa ya vikao vinavyotakiwa kufanyika hususan kikao cha kupitisha Bajeti ya Mkoa ili wajumbe wake wapate muda wa kuchangia mawazo yao kwa lengo la kuiboresha bajeti hiyo. Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Lucas Mwaisaka amekiri kuwa vikao vya Baraza hilo havijafanyika kwa muda mrefu kwa sababu mbalimbali hata hivyo  ameahidi kuwa vikao vya Baraza hilo kuanzia sasa vitatekelezwa kikamilifu na kwa mujibu wa sheria ya vikao hivyo.

Kabla ya Mgeni rasmi kuzindua Baraza hilo, ulifanyika uchaguzi wa Katibu na Katibu Msaidizi wa Baraza hilo kwa kuwa kimuundo Mwenyekiti  wa Baraza ni Katibu Tawala wa Mkoa. Katika

uchaguzi huo Bi. Angela Mono amechaguliwa kuwa Katibu na Bw. Emannuel Mazengo amekuwa Katibu Msaidizi. Wachaguliwa wote ni watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.  

Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa lina majukumu mengi mojawapo ni kushauri Mpango wa Bajeti ya Mkoa, na linaundwa na Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ndiye Mwenyekiti, Wakuu wote wa Idara na Vitengo, Makatibu Tawala wa Wilaya, wajumbe wa kuchaguliwa na wajumbe kutoka TUGHE Taifa, Mkoa na Wilaya.  



Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

    March 03, 2021
  • Wahasibu Halmashauri za Morogoro waonywa.

    March 03, 2021
  • Mkoa wa Morogoro wajipanga kuwa wa kiutalii.

    February 26, 2021
  • RC SANARE: NENDENI MKAJIFUNZE MALINYI.

    February 26, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.