Jafo: Halmashauri zote nchini undeni mabaraza ya watu wenye Ulemavu.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Mhe. Selemani Said Jafo ameziagiza Halmashauri zote nchini kuunda mabaraza ya watu wenye ulemavu yatakayo shughulikia na kutatua kero mbalimbali zinazo kabili kundi la watu wenye Ulemavu, Wazee na Watoto wa mitaani.
Waziri Jafo alisema hayo mwanzoni mwa wikii hii wakati akizungumza na wadau wa ustawi wa jamii wakati wa kuzindua mkutano uliowakutanisha wadau wote kutoka mashirika mbalimbali na asasi za kiraia zinazotoa na kushughulikia huduma za ustawi wa jamii kote nchini, mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya Edema Mjini Morogoro.
Aidha Mhe. Jafo alifafanua kuwa mkutano huo Unalenga kupitia rasimu ya mfumo na mipango ya bajeti ya mamlaka ya Serikali za mitaa utakaopanga namna ya kusaidia Makundi ya watu wenye uhitaji.
“Tutapitia maoni yote ya wadau wetu kutoka serikali na sekta binafsi ili tupate njia nzuri ya kusaidie kundi hili la watu wenye Ulemavu,Wazee na Watoto wa mitaani na lazima tujiulize kama sisi wote tuko hapa kwanini watoto wa mitaani wanatokea”.Alisema Mhe. Jafo.
Pia Waziri huyo alisisitiza kuwa katika pesa wanazopata Halmashari aslimia 10 kwajili ya mfuko wa Vijana na Wanawake ni vema watu wenye ulemavu wakatengewa asilimia 2 kutoka kwenye mfuko huo.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe S. Kebwe alisema kwa Mkoa wa Morogoro pekee watoto wanaoishi katika mazingira magumu wapo zaidi ya elfu kumi na sita (16000) ambao wanahitaji kusaidiwa.
Vile vile Mhe. Kebwe aliongeza kuwa familia nyingi ndizo zinazo sababisha wimbi kubwa la wahitaji kuongezeka pindi ndoa zinapo vunjika, akitolea mfano kwa mkoa wake Dkt. Alisema..
“kulingana na usajili wa ndoa tulionao kwa Mkoa wetu kwa mwezi Aprili hadi Juni kulikuwa na mitafaluku zaidi ya mianne (400) kwenye ndoa na kinala ni Wilaya ya Kilosa kesi zikiwa 106”
Nae Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afya za Ustawi wa jamii na lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Rashid Mafutaa amewashukuru USAID pamoja na Ps3 kwa kudhamini mkutano huo utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Tar 24 Julai Mwaka huu hadi Julai 26/2018.
Mwisho....
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.