Na. Andrew Chimesela, Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Nchini (NIDA) kufika Mkoani Morogoro ili kumaliza tatizo la msongamano wa wananchi wanaohitaji kupata vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Rais Magufuli ameyasema hayo Novemba 20 mwaka huu akiwa eneo la Msamvu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro aliposimama kuwasalimia wananchi wa Halmashauri hiyo akiwa safarini kuelekea Jijijini Dodoma.
Aidha, Dkt. Magufuli akiwa katika Mji mdogo wa Gairo amebainisha kwamba Serikali yake haitampangia mkulima bei ya kuuzia mahindi akisisitiza kwamba lazima biashara hiyo iwe huru ili kuwa na tija kwa Mkulima.
“nataka mkulima ashangilie bei ya mahindi ,wakati wa kumpangia Mkulima bei ya mahindi umekwisha, bei ya mahindi itajipanga yenyewe”, alisema Dkt. Magufuli.
MWISHO
Haki Miliki © 2018 Mkoa wa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa