• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mkurugenzi, Watumishiwatakiwakushirikiana

Posted on: September 9th, 2019

Na. Andrew Chimesela - Morogoro

Watumishi wa Halmashauri ya Wiaya ya Gairo Mkoani Morogoro wametakiwa kushirikiana katika kuinua taaluma sambamba na kuboresha miundombinu ya Elimu katika Halmashauri yao.

Ushauri huo umetolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joyce Baravuga wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ambapo alitembelea shule za Sekondari Njungwa na Nongwe ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoani humo.

Ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kukagua maendeleo ya shule za Sekondari kupitia vigezo 21 vya kutathimini utendaji kazi shuleni ili kwenda sambamba na Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro kutaka kufahamu sakata la kuuzwa bati zilizonunuliwa kwa fedha ya Serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika Shule hizo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo Agnes Mkandya alikiri kuwepo kwa sakata ambalo lilimfanya kumvua madaraka ya Ukuu wa shule na kuwa mwalimu wa kawaida kwasababu ya kukiuka taratibu za Serikali na matumizi mabaya ya mali za Serikali licha ya kuwa hilo lilifanyika kwa lengo la kulipa madeni yaliyotokana na ujenzi wa shule hiyo.

“nikweli tatizo hilo limetokea ambapo kulikuwepo bati ambazo zilibaki baada ya kukamilika ujenzi wa madarasa matatu na nyumba za walimu katika shule hizi, lakini wakuu wa shule waliuza bati hizo wakidaikulikuwepomadeni ya mafundi waliojenga majengo hayo pasipo kufahamu mali ya Serikali huwa haiuzwi”, Alisema Mkandya.

Mhandisi Baravuga pamoja na lengo la kukagua maendeleo ya shule hizo kitaaluma kupitia vigezo 21 alilazimika pia kutatua mgogoro uliopo kati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo na Wakuu wa Shule za Sekondari za Nongwe na Njungwa ambao walisimamia Ujenzi uliokuwa unaendelea katika shule zao na kuvuliwa madaraka yao.

Mhandisi Baravuga aliwataka walimu hao sambamba na Mkurugenzi wao ambaye ndiye kiutendaji ni bosi wao kushirikiana na kuhakikisha wanainua kiwango cha taaluma katika shule hiyo na Wilaya yao kwa jumla.

Ziara hiyo ya Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro ni mwendelezo wa ziara zake katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro zenye lengo la kukagua maendeleo ya shule na kufikisha vigezo 21 vya kutathmini maendeleo na utendaji kazi shuleni ambapo tayari ameshatembelea Halmashuri za Wilaya za Kilombero na Kilosa.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • NIMR YAANZA TAFITI ZA KUTIBU MALARIA.

    January 22, 2021
  • RC Morogoro atoa siku 11.

    January 21, 2021
  • WANACHI KIJIJI CHA WAMI LUHINDO WAHAMASIKA KUJENGA SHULE, WAOMBA SIKU YA HARAMBEE IPANGWE KARIBU.

    January 17, 2021
  • Miradi 67 ya maji kutekelezwa Morogoro.

    January 15, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.