Mwenge wa Uhuru umemaliza mbio zake Wilayani Gairo kwa Mafanikio.
Mwenge huo umetembelea miradi ya maendeleo ipatayo sita na Kiongozi wa Mbio za mwenge huo kuikubali na kupongeza.
Hata hivyo ameagiza Mkandarasi anayejenga majengo matano ya Kituo cha Afya cha Gairo kukamilisha kazi hiyo ifikapo Agosti 15 mwaka huu na kumtaka DC Gairo kusimamia agizo hilo.
Hii imetokana na kuchelewa kukamilisha majengo hayo ambayo yalitarajiwa hadi Juni yawe yamekamilika. Mradi huo ulitengewa sh. 400mil. kuboresha miundombinu ya kituo hicho ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa Wodi ya akinamama,jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti nala maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.