• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro achukizwa na matumizi mabaya ya michango.

Posted on: January 11th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ametishia kumfukuza kazi Mtendaji wa Mji Mdogo wa Mikumi Ndg. Mrisho Mrisho kutokana na kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya wananchi wanaogoma kutoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Sekondari Mikumi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani humo.

Loata Sanare amesema hayo Januari 10 mwaka huu ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari  Mkoani humo ambapo kwa mara nyingine alirudi katika shule ya Sekondari ya Mikumi kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa Januari 6 mwaka huu la kukamilisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa kama limetekelezwa.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sante akizungumza na Wenyeviti wa Vitongoji juu kukamilisha ujenzi wa vyumba  vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mikumi.

 Kurudi kwa Loata Ole Sanare shuleni hapo kunatokana na taarifa kuwa baadhi ya wenyeviti wa Vitongoji wa Mji Mdogo wa Mikumi kutumia tofauti na malengo yaliyokusudiwa fedha za michango zinazokusanywa kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalipia ada watoto wao kwa madai ya kurejesha fedha hizo baada ya watoto wao kupokelewa shuleni

.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare akitoa zawadi ya pesa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidoma Mlimani ambaye pia ni Makamu Menyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mikumi Bw. Salehe Tangula kwa kuhamasiha wananchi kushiriki katika maendeleo ya ujenzi wa shule ya Sekondari Mikumi.

‘’kuna pesa zimeliwa, kuna pesa zimekusanywa kwa wananchi na ndiyo sababu nagombana na watendaji, kwanini msikusanye, wengine wamekusanya wakasema tunawapeleka watoto wetu shule baadae tutakuja kupambana kutafuta pesa tulizokusanya” amesema  Sanare.

Katika  hatua nyingine Mkuu  wa Mkoa wa Morogoro amempongeza Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidoma Mlimani ambaye pia ni Makamu Menyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mikumi Bw. Salehe Tangula kutokana na kazi nzuri ya kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wananchi kushiriki kazi za maendeleo, ukusanyaji wa michango kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuwasilisha kwa wakati fedha za michango kwa Kiongozi wake.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo akimpatia zawadi na mkono wa pongezi Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kidoma Mlimani ambaye pia ni Makamu Menyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mikumi Bw. Salehe Tangula kwa kazi nzuri ya uhamasishaji wananchi kushiriki kazi za maendeleo.

Loata amebainisha kuwa vyema kuwa mkali pale ambapo kiongozi anashindwa kutekeleza wajibu wake lakini pia kutoa pongezi na kusifia pale ambapo kuna jitihada za kutekeleza majukumu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Karibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiwasisitiza wananchi Mji Mdogo wa Mikumi kuwa wazalendo katika kufanya shughuli za maeñdeleo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amewataka wananchi wa Mji Mdogo wa Mikumi kuwa na moyo wa uzalendo katika kujitolea kufanya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo hadi sasa unaonekana kusuasua.

Mhandisi Kalobelo amesema ni aibu kwa wananchi wa Mji wa mikumi kujenga msingi wa vyumba vya darasa kwa kutumia tofali za kuchoma badala ya kujengwa kwa mawe  au matofali ya saruji huku akidai huko ni kukosa uzalendo na kutopenda maendeleo yao.

“…Watu hawapendi maendeleo yao tumeenda sehemu tumekuta misingi ya madarasa inajengwa kwa mawe au tofali za block, lakini hapa mmeokoteza haya matofali, na sehemu zote hata vijijini wamejenga madarasa mengi zaidi  siyo Mjini kama hapa Mikumi…” amesema Kalobelo

Mwonekano wa ujenzi wa vyumba  vya madarasa vya Shule ya Sekondari Mikumi  ambao unapelekea Mkuu wa Mkoa Loata Sanare kuwa mkali kwa viongozi wa Mji Mdogo Mikumi kutokana na kutotimiza wajibu wao wa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Januari 6, mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare alimuagiza Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Kilosa kuwaweka rumande wenyeviti wa vitongoji 21 katika Mji Mdogo wa Mikumi kwa kushindwa kuhamasisha wananchi kushiriki ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vinavyohitajika kwa ajili ya wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza  wanaotarajiwa kuanza masomo yao Januari 11 mwaka huu.


MWISHO 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Miradi 67 ya maji kutekelezwa Morogoro.

    January 15, 2021
  • Maafisa Ugani Morogoro watakiwa kuongeza jihudi, wapatiwa pikipiki.

    January 14, 2021
  • Mwenyekiti wa Kijiji mbaroni kwa kuuza Ardhi..

    January 13, 2021
  • RC Morogoro atembelea soko Kuu la Manispaa, atoa maelekezo.

    January 12, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.