• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro ampongeza JPM.

Posted on: October 26th, 2019


Andrew Chimesela – Morogoro.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuthubutu kutekeleza kwa Vitendo mradi wa kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Mhe. Loata ametoa pongezi hizo Oktoba 25 mwaka huu alipotembelea mradi wa kufua Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere {Julius Nyerere Hydropower Project – JNHPP}ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea mradi huo akiwa Mkuu wa Mkoa huo.


Akiambatana na Wajumbe wake wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoianza hivi karibuni ya kujitambulisha rasmi Mkoani humo pamoja na kuona utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Mhe Ole Sanare anafika katika mradi wa kufua umeme na kujionea kazi inavyoendelea bila kutegemea anajikuta anampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uthubutu wa kutekeleza mradi huo mkubwa na wa thamani utakaowaletea maendeleo wananchi hususan wanyonge.


“kikubwa kuliko yote ni kumshukuru sana na kumpongeza mheshimiwa Rais wetu kwa kutekeleza mradi huu ambao ulishaibuliwa enzi za Mwalimu Nyerere lakini haukuweza kutekelezwa sasa amekuja yeye amesema ni ‘take Off’ sasa (nianze kutekeleza) ni mradi wa siku nyingi sana…” alisema Ole Sanare.

“tumpongeze na kumshukuru sana kwa kufuata nyayo za baba wa Taifa hili yeye amesema yale yote ambayo aliyabuni atayatekeleza na yanatekelezeka” amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha, amewataka wahandisi wazawa wanaosimamia utekelezaji wa mradi huo ambao wanafikia asilimia tisini ya wahandisi wote wanaofanya kazi katika mradi huo, kusimamia kwa uadilifu mradi huo na kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pamoja na pongezi hizo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ameweka wazi kuwa Ofisi yake iko tayari kushirikiana kwa karibu na wakandarasi na wahandisi wa mradi kwa huo kila changamoto itakayojitokeza ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kwa malengo yanayotarajiwa.

Pamoja na kukiri kasi nzuri ya mradi huo, Mhe. Ole Sanare ameahidi Kamati yake ya Ulinzi na Usalama itaweka ratiba ya kuutembelea mradi huo kila baada ya miezi miwili ili kujiridhisha kazi inavyoendelea pamoja na kuimarisha Amani ya eneo nzima la mradi.

Katika hatua nyingine Mhe. Ole Sanare wakati wa ziara hiyo alisimama kwa muda eneo la Kisaki ambalo ni kituo kikubwa kilichopo karibu na mradi huo na kutumia dakika kadhaa  kuongea na wananchi wa eneo hilo.

Katika hotuba yake amewataka Vijana zaidi ya elfu moja kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini waliofika eneo la Kisaki kwa ajili ya kutafuta kazi  kwenye mradi wa bwawa la kufua umeme, kurudi nyumbani kwao ili kutoa nafasi ya eneo la Kisaki kutokuwa na watu wengi kuliko uwezo wake.

Pamoja na agizo hilo kwa vijana  kurejea makwao na kurejea hapo watakapohitajika, ameviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo kuimarisha Usalama katika eneo la kisaki masaa ishirini na Nne huku akiwataka wanaoshughulika na kupokea vijana kwenye mradi huo kutenda haki katika kuwapokea vijana hao.

Naye Mratibu wa Mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere Mhandisi Stephen Manda ameeleza hatua ya mradi huo akibainisha kuwa wako ndani ya ratiba lakini pia kazi nyingine ziko mbele ya wakati. Amesema lengo lao ni kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa yaani mwezi Juni 2022.

Hata hivyo amewaomba wadau wanaofanyakazi nao na watanzania wote kwa jumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwao ili watekeleze kazi hiyo kwa wakati huku akitoa wito kwa Wakuu wa Mikoa ya Morogoro na Pwani ambayo mradi huo upo kuendelea kusimamia suala nzima la Amani ili wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi huo wafanye kazi zao kwa ufasaha na ufanisi.

Kwa upande wake Onesmo Sanga ambaye ni dereva wa Mitambo mikubwa anayetafuta kazi katika eneo hilo la mradi wa kufua umeme, ameiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA kuwasaidia kupata namba za vitambulisho ili ziwasaidie kupata kazi katika mradi huo kwa kuwa wengi wao  hadi sasa hawana vitambulisho hivyo na kuwa moja ya changamoto kubwa katika kupata kazi.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • RC SANARE ATATUA MGOGORO WA ARDHI.

    April 13, 2021
  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.