• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC SANARE AAGIZA TAKUKURU KUFANYA UCHUNGUZI WA MIL. 260

Posted on: January 24th, 2021

Mkuu Wa  Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo kuchunguza ubadhilifu wa fedha za mradi wa ujenzi  wa Mabweni mawili ya wasichana na bwalo la chakula katika shule ya Sekondari ya Gairo.

 Loata Sanare ametoa agizo hilo Januari 24 mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Gailo alipotembelea Shuleni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule hiyo.

Loata Sanare amesema hakuna sababu yoyote ya msingi ambayo imepelekea kutokamilika kwa ujenzi huo kwa kuwa Serikali imepeleka Shilingi 260 Mil. Kwa ajili ya ujenzi huo ambapo shilingi milioni 160 ni kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili na shilingi milioni 100 kwa ajili ya bwalo la chakula.

Katika hatua nyingine, Loata Sanare ametoa wiki moja kwa TAKUKURU  kufanya uchunguzi wa mradi huo na kuwasilisha taarifa yake katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kabla au ifikapo Januari 29 mwaka huu ili kuwachukulia hatua wale watakaobainika kufanya ubadhilifu wa matumizi ya fedha hizo za umma.

Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo amewasimamisha kazi wataalam  wa ujenzi wa  mradi huo na kumuagiza kamanda wa jeshi la Polisi Wilaya ya Gairo (OCD) kumshikiria Mkandarasi Izengo Majija ambaye anahusika na usimamizi wa ujenzi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU Mkoani hapa Janeth Machulya amebainisha kuwa hadi sasa uchunguzi umeanza kufanyika  ili kubaini matumizi yasiyo halali ya fedha hizo, kisha watawasilisha taarifa ya uchunguzi huobaada ya kukamilika.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Gairo  Zainab Yambi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa Shule hiyo, amesema kamati yake ilikuwa ikihusika na kupitisha vifaa vinavyohitajika kutoka kwa wataalam wa ujenzi kisha kufikisha mahitaji hayo kwenye kamati ya manunuzi na baada ya manunuzi kuwasilisha vifaa hivyo kwa wataalam hao kwa ajili ya kuendelea na kazi.

Ujenzi wa mradi wa mabweni mawili ya wasichana na bwalo moja la chakula ulianza Julai 2020 na ulitakiwa kuamilika Oktoba 2020, hata hivyo hadi sasa ujenzi huo umefanyika kwa asilimia 40 tu licha ya Serikali kupeleka shilingi 260 Mil. kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • ZAIDI YA BIL. 7 ZATARAJIWA KUTUMIKA MOROGORO.

    March 04, 2021
  • Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

    March 03, 2021
  • Wahasibu Halmashauri za Morogoro waonywa.

    March 03, 2021
  • Mkoa wa Morogoro wajipanga kuwa wa kiutalii.

    February 26, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.