• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC SANARE: NENDENI MKAJIFUNZE MALINYI.

Posted on: February 26th, 2021

Halmashauri za Mkoa wa Morogoro zimetakiwa kujifunza mbinu za ufundishaji ambazo zimetumiwa na  Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kuwafundisha wanafunzi nakufanikisha  kushika nafasi  ya kwanza Kimkoa na ya tisa kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2020.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare katika hafla iliyofanyika Februari 23 mwaka huu kwa ajili ya kuzipongeza  shule zilizofanya vizuri Wilayani humo katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba ya mwaka 2020.

‘’Lakini nawahakikishia mmenipa  jambo la kuzungumza, kila ninapopita nawambia nendeni mkajifunze kule Malinyi, nyinyi watu wa Manispaa nyie watu mnaokaa karibu na Manispaa mmeshindwa na watu wanaoitwa wa porini’’ amesema Sanare.

Aidha, Loata Sanate ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuupa heshima Mkoa wa Morogoro na kuufanya kutambulika, licha ya changamoto mbalimbali  za kielimu zilizokuwepo bado Halmashauri hii ya Malinyi imeibuka kuwa ya kwanza  na kuzishinda Halmashauri nyingine za Mkoa huo.

Hata hivyo, Loata Sanare ametoa wito kwa Halmashauri hiyo kuongeza jitihada katika ufundishaji ili waweze kubaki katika nafasi hiyo ya kwanza huku akiwasisitiza kutobweteka kutokana na kushika nafasi hiyo  badala yake wajipange vizuri ili mwakani  waweze kutetea nafasi yao.

Awali, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Loata Ole Sanare, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Masele amesema Halmashauri hiyo itaendelea kufanya vizuri kama ambavyo imefanya mwaka jana na kuendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba sekta ya Elimu katika Halmashauri hiyo ili zisiwe kikwazo kwa matokeo yajayo.

Akibainisha mpango mkakati wa kuendeleza kufanya vizuri katika Sekta ya Elimu, Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Linda Malandu amesema, Halmashauri hiyo imejipanga kudhibiti utoro kwa wanafunzi,  kuhamasisha walimu kujiendeleza kitaaluma na kuendelea kuhimiza wazazi kuhusu uchangiaji wa chakula kwa wanafunzi ili waweze kupokea maarifa vizuri wawapo darasani.


Akizungumzia changamoto zinazoikumba Halmashauri hiyo katika Upande wa Elimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Hawa Mposi amesema Halmashauri hiyo ina upungufu wa walimu 417 kati ya 800 wanaohitajika Wilayani humo.

Mkoa wa Morogoro umeshika nafasi ya nane kitaifa katika  matokeo ya mtihani wa Taifa darasa la saba mwaka 2020, huku Halmashauri ya wilaya ya Malinyi imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya Halmashauri tisa za mkoa huo sawa na asilimia 96 za ufaulu.


MWISHO


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • RC SANARE ATATUA MGOGORO WA ARDHI.

    April 13, 2021
  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.