• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Uingereza kuwekeza Mkoani Morogoro.

Posted on: July 19th, 2018

Uingereza kuwekeza Mkoani Morogoro

 

Na. Andrew Chimesela - Morogoro

Serikali ya Uingereza imeonesha nia ya kushawishi wawekezaji nchini mwake kuja kuwekeza hapa nchini hususan katika Mkoa wa Morogoro katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Kilimo, viwanda na Madini.

Hayo yamefahamika jana Julai 18 mwaka huu wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro baina ya Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Bi. Sarah Cooke na Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa huo.

Awali viongozi hao wawili walianza mazungumzo yao kuhusu miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Uingereza hapa nchini hususan iliyopo Mkoani Morogoro ikiwemo miradi ya Elimu - Educationa Programme for Results (EP forR), ambapo Mhe. Cooke alisema nchi yake imeongeza ufadhili wake kutoka 34% mwaka 2012 hadi 70/% mwaka 2016.

Kwa upande wa Afya Balozi huyo alisema katika Mkoa wa Morogoro, Uingereza imefadhili Vituo vya Afya katika eneo linalolenga Mpango wa Uzazi kwa akina mama kupitia Mradi wa Population Service International (PSI) ambapo hadi sasa jummla ya akinamama 9,400 Mkoani humo wamefaidika na huduma hiyo.

Aidha, Viongozi hao wawili walizungumzia ufadhili unaotolewa na Uingereza katika nyanja za Maji na Usafi wa Mazingira ikiwemo Kampeni inayoendelea sasa Mkoani Morogoro ya usichukuliepoanyumbanichoo, Mkoa huo ukiwa ni Mkoa wa Majaribio katika Kampeni hiyo.

Pamoja na miradi mingine mingi waliyoizungumzia , Viongozi hao pia waligusia miradi ya Sekta ya Kilimo na Miundombinu. Kwa upande wa Sekta ya Miundombinu upo mradi wa IRAT yaani Improving Rural Access in Tanzania ambapo Uingereza imefadhili matengenezo ya makaravati ya barabara ya Chagongwe - Kumbulu iliyopo Wialaya ya Gairo.

Baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu miradi inayofadhiliwa na nchi ya Uingereza, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe alimshukuru Balozi wa Uingereza kwa Ufadhili wa miradi yote hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa Upimaji na umilikishaji wa Ardhi unaotekelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kupitia Land Tenure Support Programme. 

Dkt. Kebwe ametumia fursa hiyo kumweleza Balozi Sarah Cooke uwepo wa maeneo mazuri ya uwekezaji katika Mkoa wa Morogoro na akawasilisha ombi kwa balozi huyo kushawishi wawekezaji walioko nchini mwake kuja kuwekeza Mkoani Morogoro katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Kilimo, viwanda na uchimbaji wa madini ya dhahabu na Graphite.

Balozi Sarah Cooke alionekana kushawishika na ombi la mwenyeji wake na kuahidi kulifanyia kazi haraka huku akiahidi kutafuta muda wa kufanya ziara katika Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kutembelea miradi wanayoifadhili lakini pia kutembelea maeneo ya uwekezaji kama alivyokuwa ameombwa na mwenyeji wake.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Serikali inapoteza Bil. 18 kwa mwaka

    March 03, 2021
  • Wahasibu Halmashauri za Morogoro waonywa.

    March 03, 2021
  • Mkoa wa Morogoro wajipanga kuwa wa kiutalii.

    February 26, 2021
  • RC SANARE: NENDENI MKAJIFUNZE MALINYI.

    February 26, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.