Barabara ya Morogoro – Dodoma kukamilika usiku
Na Andrew Chimesela, Morogoro
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema daraja la Mto Mkenge lililopo Wilayani Kilosa lililovunjilka Machi 2 mwaka huu, linatarajiwa kukamilika usiku wa kuamkia Machi 4 mwaka huu.
Waziri Kamwelwe amesema hayo akiwa katika eneo la tukio, mara baada ya Karavati moja kati ya mawili yanayohitajika kushushwa sehemum lilipokatika daraja na kutoa matumaini kuwa ujenzi wa daraja hilo la muda utakamilika usiku wa kuamkia Machi 4 Mwaka huu.
Hata hivyo Waziri amesema kuwa daraja hilo kwa sasa halitapitisha magari mawili kwa pamoja badala yake gari moja tu litaruhusiwa kupita hadi hapo utaratibu mwingine utatakapotolewa.
Aidha, Waziri amesema karavati la awali ambalo limevunjika lilikuwa na kipenyo cha Mita tatu tu na sasa yamewekwa makaravati mawili kila moja likiwa na kipenyo cha Mita tatu hivyo kuruhusu maji mengi kupita tofauti na awali.
Akitoa matumaini kwa watanzania hususana madereva watakaotumia barabara hilo la Morogoro – Dodoma Waziri amesema kazi ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo utaendelea mara baada ya mvua kupungua.
Kwa upande waka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha tangu adha hiyo ilipotokea hususan madereva kwa kutii maelekezo ya Serikali walipotakiwa kubaki maeneo walipo hadi watakapoelekezwa vingine.
Daraja la Mto Mkange lililopo katika Kijiji cha Kiegeya Wilayani Kilosa lilivunjika Machi 2 Mwaka huu majira ya saa kumi jioni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na Usafirishaji.
MWISHO
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.