WAHANGA WA MAFURIKO KILOSA WAENDELEA KUPOKEA MISAADA, DC KILOSA ATOA WITO KUWASAIDIA
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wahanga wa mafuliko yaliyotokea wilayani humo na kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu makazi ya wanachi na kusomba mazao yaliyokuwa shambani.
Mhe. Mgoyi akiambatana na Watafiti wa Kilimo kanda ya Mashariki ARI Ilonga mwanzoni wa wiki hii wametembelea maeneo mbalimbali yaliyo athirika na kutoa michango ya mbegu za mihogo pingili 35,000, Mbaazi kg 100, Kunde kg 50, Alizeti kg 60, kwa upande wa chakula wametoa Mihogo ya chakula Tani 2.1 na Mahindi 2.7 pamoja na Sukari na Chumvi.
Aidha , Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo kanda ya Mashariki ARI Ilonga Dkt. Geofrey Mkamilo amesema kuwa wameguswa na tukio la mafuriko hayo na kwamba wako bega kwa bega na Halmashauri pamoja na Wilaya kwa ujumla ilikuhakikisha suala la mbegu linakaa sawa na kwamba wameamua kutoa mbegu za mihogo na mihogo ya chakula.
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimesababisha mafuriko baadhi ya Mikoa ikiwemo Mkoa wa Morogoro katika Wilaya ya Kilosa ambako imeharibu miundo mbinu ya reli, barabara, pia mafuriko yameharibu mazao yaliyokuwa mashambani pamoja na kuharibu makazi ya wananchi.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.