Jumla ya Wanafunzi 1,194 wa Shule za Msingi na Sekondari Katika Mkoa wa Morogoro wamepata Mimba katika kipindi cha Miaka Minne (2016-2019) nakukatiza ndoto zao za Kusoma
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa Morogoro Loata Ole Sanare Septemba 15 Mwaka huu katika kikao kilicho wahusisha Viongozi mbalimbali wa Mkoa huo wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa na Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro.
“Suala la Wanafunzi wetu kupata mimba wakiwa shuleni bado ni tatizo kubwa katika Mkoa wetu. Mwaka 2016 jumla ya Wanafunzi 37 wa Msingi na 204 wa Sekondari walipata Mimba, Mwaka 2017 idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia Wanafunzi 67 wa msingi na 237 wa Sekondari. Kama vile haitoshi mwaka 2018 idadi hiyo ilipanda zaidi na kufikia wanafunzi 76 wa Masingi na 255 wa Sekondari kupata mimba. Mwaka 2019 Wanafunzi wa Msingi waliopata mimba walifikia 69 na Sekondari 169”amesema Sanare
Aidha, amesema mpaka sasa baadhi ya watuhumiwa waliowabebesha Mimba Wanafunzi hao wameshakamatwa na kufikishwa katika vyombo husika kujibu mashitaka yanayo wakabili.
Hata hivyo Sanare amesema Mkoa wa Morogoro umedhamiria kuboresha elimu katika Ngazi zote za Msingi na Sekondari kwa nia ya kuinua kiwango cha ufaulu katika Mitihani ya Taifa.
” Takwimu tulizo nazo tuna kazi ya kumalizia maboma ya miundombinu ya elimu msingi na Sekondari kama ifuatavyo: Vyumba vya madarasa 192, Nyumba 69 za Walimu shule za msingi, vyumba 138 vya madarasa shule za Sekondari, nyumba 57 za walimu wa Sekondari, Mabweni 12, Vyumba vya maabara za Sayansi 355”amesema Sanalele
Pia Sanale amesema Ujenzi wa Mabweni kwa Wanafunzi utasaidia kutatua changamoto ya Mimba ambazo zimekuwa changamoto za kutowatimizia wanafunzi ndoto zao na kuwataka Wazazi kuwa na utaratibu wakufuatilia mienendo ya watoto .
MWISHO
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.