• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Zaidi ya Bil. 7 kutumika ujenzi wa Miundombinu Mkoani Morogoro

Posted on: October 22nd, 2020


Na Andrew Chimesela, Morogoro

Zaidi ya shilingi Bil. 7 za kitanzania zinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja Mkoani Morogoro kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Hayo yamebainishwa  Oktoba 22 mwaka huu na Mratibu wa Wakala wa Barabara Vijijini TARURA Mhandisi Benjamini Maziku wakati wa hafla fupi ya kusaini mikataba ya miradi 35 kati ya 46 iliyotangazwa kutekelezwa Mkoani humo.

Baadhi ya viongozi wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya miradi mbalimbali Mkoani Morogoro. kutoka kulia ni Mratibu wa TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Benjamini Maziku, Mhandisi Emmanuel Kalobelo(RAS) na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Miundombinu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ezron Kilamhama

Kwa mujibu wa Mratibu huyo ametaja idadi ya miradi hiyo itakayotekelezwa kwa kipindi hicho kwa kila Halmashauri na thamanai yake kwenye mabano kuwa ni pamoja na Wilaya ya Gairo miradi 3 (437,489,610.00), Ifakara miradi 3(370, 135,786.00), kilosa 5(Tsh. 887,694,910.00) na Kilombero 3(Tsh. 350,300, 340.00).

Baadhi ya wakandarasi, mameneja wa TARURA na Washiriki wa hafla hiyo

Miradi 6 ya Morogoro vijijini (Tsh. 850,904,100.00), Mvomero miradi 8(Tsh. 583,582,360.00) Malinyi mradi mmoja (Tsh. 167,154,000.00, na Halmashauri ya Manispaa Morogoro 5(Tsh. 1, 598,275,495.00)

Akifungua kikao hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka TARURA kuwa na utaratibu wa  kuwalipa kwa wakati wakandarasi wanaoingia nao mikataba katika miradi mbalimbali ili wakandarasi hao waweze kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo akiongea na Wakandarasi na Mameneja wa TARURA wa Halmashauri wakati wa hafla fupi ya kusaini Mikataba

Mhandisi Kalobelo amesema hatua ya kuwalipa mapema wakandarasi hao itasaidia kuwasukuma wakandarasi katika utendaji kazi wao wa kutaka kukamilisha miradi yao kwa wakati bila kuwa na kigugumizi kwa kuwa tayari watakuwa hawana hoja ya kujitetea “Ili tuweze kuwabana hao wakandarasi vizuri na sisi TARURA …..tunapowapa Wakandarasi kazi pia tutimize wajibu wetu kwa kuwalipa kwa wakati” alisema Mhandisi Mhandisi Kalobelo.

Baadhi ya Wakandarasi na Meneja wa TARURA wakimsikiliza Mhandisi Kalobelo

Kwa upande wa Wakandarasi Katibu Tawala huyo amesema kama wapo Wakandarasi wenye tabia ya kutokamilisha kazi zao kwa wakati waone aibu na mara watakapo saini mikataba hiyo wawasilishe mipango kazi yao kwa TARURA na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya ufuatiliaji.

Kwa upande wao Wakandarasi hao wakiwakilishwa na Mhandisi Stanslaus Mkude wa Kampuni ya Luba Contractors pamoja na kuishukuru Serikali kwa kuwaona wanafaa kufanya kazi nao na kuwasihi wakandarasi wenzake kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kwa kuzingatia muda, huku akiwashawishi wenzake kuwatoa wafanyakazi wasiowajibika ipasavyo na kuwaajiri wengine kwa muda ili lengo la kukamilisha kwa wakati miradi husika liweze kutimia hivyo kuaminiwa na Serikali.

Hii ni baadhi ya Mikataba ya Miradi mbalimbali inayosubiriwa kusainiwa

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • RC SANARE ATATUA MGOGORO WA ARDHI.

    April 13, 2021
  • Morogoro kumuenzi JPM kwa kudumisha Amani na Utulivu.

    March 24, 2021
  • RC MSTAAFU STEVEN MASHISHANGA ATOA SALAMU ZA POLE.

    March 19, 2021
  • RC Sanare awapa pole Wanamorogoro kwa Msiba Mkubwa, awataka watulie

    April 28, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.