TEHAMA

Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano


Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina lengo la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa Sekretarieti ya Mkoa, Aidha Kitengo hiki kinaongozwa na Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa. 


Majukumu ya Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Majukumu ya Idara/Seksheni

Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

  • Kutayarisha mpango Mkakati wa kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano, Miongozo na taratibu kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
  • Kuishauri Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa juu ya masuala yanayohusiana na sera zinazohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wa dhana ya serikali mtandao.
  • Kuishauri Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa juu ya masuala yanayohusiana na sera, miongozo na taratibu zinazohusiana na takwimu.
  • Kusimamia maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano na utekelezaji wake kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa.
  • Kushirikiana na OWM-TAMISEMI kuratibu na kuendeleza viwango vya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili ya “software na hardware” kwa matumizi ya Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza na kutekeleza  mipango/miradi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
  • Kuratibu utekelezaji wa usanifu na kutunza/kuiendeleza matumizi yanayohusiana na Tovuti na utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa.
  •   wizarani, Idara, wakala na wadau wengine.
  • Kutoa na kuratibu msaada wa teknolojia ya habari kwa Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Kutathimini, kuboresha na kusimamia teknolojia ya habari na mawasiliano na usimamizi wa mifumo ya taarifa/habari iliyosimikwa/iliyowekwa kwenye Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo juu ya usimamizi wa mifumo ya taarifa na teknolojia ya habari na mawasiliano na kuandaa mpango wa kujenga uwezo
  • Kufanya tathimini ya hatari/hasara zinazohusiana na miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mfumo wa usimamizi wa taarifa na namna ya kuthibiti.
  •   Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Kuendeleza na kutunza Tovuti ya Mkoa.
  • Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwenye kushughulikia takwimu na taarifa
  •   taarifa, kutunza, kuzipitisha hatua mbalimbali, kuzichambua, kuziwasilisha, kuzisambaza na kuzihifadhi.
  • Kushirikiana na Tume ya Taifa ya Takwimu juu ya masuala yote yanayohusu Mfumo wa Taifa wa Takwimu.
  • Kuandaa masuala yote yanayohusiana na takwimu kwenye Sekretarieti ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.