Utawala na Rasilimali Watu

Jeshi la Mgambo

Jeshi la Mgambo Mkoani limeendelea kuimarishwa na kuboreshwa kwa kutoa mafunzo kwa wananchi  wake . Lengo ni kutoa mafunzo kwa wanamgambo 600 kila mwaka utekelezaji ni kama ifuatavyo;-

S/N

Mwaka

Lengo

Utekelezaji

Ongezeko/Pungufu

1.

2010/11

600

690

90

2.

2011/12

600

616

16

3.

2012/13

600

492

-108

4.

2013/14

600

531

-69

5

2014/15

600

640

40

Wanamgambo wanashirikiana vyema na vyombo vingine vya Usalama katika kudumisha amani na utulivu Mkoani. Aidha dhana ya ulinzi shirikishi jamii imesaidia sana katika kuboresha ulinzi.

Mapambano dhidi ya Rushwa

Mkoa umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita na kukemea vitendo vya RUSHWA kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Jamii imeendelea kuhamasishwa na kuelimishwa juu ya athari za rushwa na madhara yake katika jamii na Taifa zima kwa ujumla.

Mwenge wa Uhuru

Katika kipindi chote nilipokuwa hapa, Mwenge wa Uhuru ulikuwa ukipita na kukimbizwa Mkoani kwa mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kufikisha jumbe mbalimbali za Mwenge wa Uhuru. Mwenge kila unapokimbizwa umeweza kusaidia kuendeleza umoja na mshikamano wa wananchi kwani wamekuwa washiriki pamoja bila kujali itikadi zao za kisiasa, kidini,  hali zao n.k.  Mwenge pia umekuwa ni kichocheo cha kuwezesha miradi ya maendeleo kutekelezwa haraka,  kutoa elimu na ujumbe maalumu kwa wananchi kote ulikopita. Taarifa ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2012 inaonesha kuwa, Mkoa ulishika nafasi ya kumi ( 10 )  kitaifa na mwaka 2013 ulishika nafasi ya Nne ( 4 ) kitaifa kati ya Mikoa 30 iliyopo nchini. Kwa mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru utapokelewa kutoka Mkoa wa Tanga na kukabidhiwa Mkoa wa Iringa.

Watumishi wa Mkoa

Mpaka tarehe 15 Desemba, 2014, idadi ya Watumishi wote katika Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa  ni 18,725. Mchanganuo wa watumishi hawa ni kama ifuatavyo:

Idadi ya Watumishi katika Mkoa

Mkoa/Halmashauri

Idadi ya Watumishi

Asilimia

Mkoa

820

5

Manispaa

3,664

16

Morogoro DC

2,854

12

Mvomero

2,986

15

Kilosa

3,868

23

Kilombero

3,483

17

Ulanga

1,050

13

JUMLA

18,725

100

Chanzo: Taarifa za Uhakiki wa Madai ya Watumishi ,2014