Serikali za Mitaa

Ugatuaji Madaraka

Kipindi cha 2008 hadi 2014 ni cha utekelezaji wa dhana ya Ugatuaji na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma ambapo hadi sasa sekretarieti za Mikoa zimekabidhiwa majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na Kanda za Maboresho.

Majukumu hayo matatu (3) ni yafuatayo:-

  • Ufuatiliaji na kuzishauri Serikali za Mitaa juu ya Uimarishaji wa Utawala Bora.
  • Ufuatiliaji na kuzishauri Serikali za Mitaa juu ya uboreshaji wa vyanzo na taarifa za mapato na matumizi ya fedha.
  •   Ufuatiliaji na kuzishauri Serikali za mitaa juu ya Uimarishaji wa Rasilimali watu na Muundo wa Halmashauri.

Uboreshaji wa Serikali za Mitaa

Mkoa wa Morogoro ulitekeleza mpango wa uboreshaji wa Serikali za mitaa awamu ya kwanza na kufanikiwa katika maeneo yafuatayo:

Kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi ya fedha .

Mtiririko wa Ukusanyaji Mapato ya Ndani kwa upande wa Mamalka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro kuanzia mwaka 2005 - 2014  ni kama ifuatavyo;-

Jedwali Na.4 Makusanyo ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa 2005 – 2014

Na.

JINA LA HALMASHAURI

MAKUSANYO 2005

MAKUSANYO 2014

ONGEZEKO

IDADI

ASILIMIA

1

KILOSA DC

169,414,751.64

1,521,953,460.33

1,352,538,708.69

88.87

2

KILOMBERO DC

267,932,375.00

3,955,995,318.00

3,688,062,943.00

93.23

3

MOROGORO DC

  334,712.56

609,980,225.61

609,645,513.05

99.95

4

MOROGORO MANISPAA

613,766,736.00

3,678,586,893.05

3,064,820,157.05

83.32

5

MVOMERO

236,118,487.69

786,096,967.00

549,978,479.31

69.96

6

ULANGA DC

  225,962,377.00 

2,386,076,135.20

2,160,113,758.20

90.53

JUMLA YA MAPATO

1,513,529,439.89

12,938,688,999.19

11,425,159,559.30

88.30

Kutunga na kusimamia sheria ndogo ili kudhibiti uvunjaji wa sheria.

Halmashauri zote na Sekretarieti ya Mkoa zimeanzisha Ofisi za kushughulikia malalamiko na kero za wananchi. Rejesta na masanduku ya maoni yamewekwa katika sehemu zote za huduma. Aidha, Ofisi zote za Tarafa, Kata na Serikali za Vijiji zinapokea malalamiko na kero za wananchi na kuzifuatilia.

Kuwashirikisha wananchi katika kupanga mipango ya bajeti kwa kutumia mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo (O & OD).

Taarifa zote za Halmashauri zinazohusu mapato na matumizi, zabuni na taarifa za miradi ya maendeleo zimetangazwa kwenye magazeti na kubandikwa katika mbao za matangazo ili kukuza dhana ya uwazi na uwajibikaji kwa wananchi na wadau wengine.

Halmashauri na Mkoa zimezingatia masuala ya jinsia katika ajira na shughuli mbalimbali za kiutumishi.

Halmashauri na Mkoa zimeunda Kamati za Kisheria na kuendesha vikao vya kamati husika kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo.

Halmashauri zote ndani ya Mkoa zimeendelea kuendesha vikao vya Serikali za Vijiji/Mitaa na mikutano ya wananchi ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utawala na uendeshaji wa mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo yao.

Mkoa wa Morogoro tayari umeunda kamati ya Ushauri ngazi ya Mkoa (RCC) na Wilaya (DCC) na kufanya vikao kila mwaka.

Matokeo ya mikakati hiyo imepelekea Makusanyo ya ndani ya Halmashauri kuongezeka kutoka sh.1,513,529,439.89 mwaka 2005 hadi kufikia sh.12,938,688,999.19 mwaka 2014. Kiasi hiki ni sawa na ongezeko la asilimia .88.30

Uandishaji Wapiga kura

Mamlaka za Serikali za Mitaa ziliendesha zoezi la kuandikisha wapiga kura katika rejesta za wakazi  kwa ajili ya uchaguzi wa Wenyeviti ngazi ya vijiji, mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za vijiji na mitaa. Zoezi hilo lilifanyika kuanzia tarehe 23 - 29 Novemba, 2014  na kufanikiwa kuandikisha wapiga kura 660,007 sawa na asilimia 74 ya lengo la kuandikisha wapiga kura 887,397 waliokisiwa.Idadi ya walioandikishwa ni sawa na asilimia 40 ya idadi ya watu 2,218,492 waliopo katika Mkoa kulinga na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. 

Uandikishaji kwa kila Halmashauri ni  kama ifuatavyo: Ulanga 84,356 (80%), Kilosa 137,769 (79%), Gairo 35,388 (47%), Mvomero 88,701 (71%), Kilombero 143,058 (88%), Morogoro 89,247 (78%) na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro 80,660 (64%). 

Katika maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Kitongoji, Mitaa na Vijiji, Sekretarieti ya Mkoa ilipokea fedha shilingi 418,486,148/- na kuzipeleka katika Halmashauri za Wilaya/Manispaa kwa mchanganuo ufuatao:-

Mgawanyo wa Fedha za uchaguzi Mkoa wa Morogoro

Na

Halmashauri

Makisio

Kiasi kilichotolewa

Pungufu

1

Gairo

91,666,000

30,274,546.

61,391,454

2

Kilombero

200,000,000

70,632,579.

129,367,421

3

Kilosa

182,805,323

69,805,323.

113,000,000

4

Morogoro

171,820,000

65,420,053.

106,399,947

5

Morogoro MC

85,000,000

52,772,079.

32,227,921

6

Mvomero

119,530,100

69,977,558.

49,552,542

7

Ulanga

155,000,000

59,604,009.

95,395,991

Jumla

1,005,821,423

418,486,147

587,335,276

Pia masanduku ya kupigia kura 7,890 yamepokelewa masanduku 6,401 yalikuwepo

hivyo jumla ya masanduku yote ni 14,291. Kwasasa kila Halmashauri ya Wilaya imeanza kusambaza masanduku kwenye vijiji kwa kuanza na vijiji vilivyo mbali na makao makuu ya Wilaya.

Kampeni za uchaguzi na uchaguzi

Kampeni za uchaguzi zilifanyika vyema  katika kata zote kwa amani na utulivu. Ratiba za kampeni ziliandaliwa kwa kushirikisha vyama vyote hivyo kupelekea kutokuwa na malalamiko. Uchaguzi ulifanyika vyema katika Wilaya zote isipokuwa mapungufu yalijitokeza katika Wilaya ya Ulanga ambapo katika Kata 8 zenye jumla ya vijiji 18 zoezi halikufanyika kutokana na kukosewa kuchapishwa kwa karatasi za kupigia kura na katika Wilaya ya Mvomero ni Vijiji viwili na Kitongoji Kimoja.

Vyama vinavyoshiriki Uchaguzi

Jumla ya vyama kumi na moja (11) vilishiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014. Vyama hivyo ni;

1. Chama Cha Mapinduzi (CCM)

2. CHADEMA

3. CUF

4. TLP

5. NCCR

6. UPDP

7. ADC

8. UDP

9. JAHAZI ASILIA

10. AFP

11. SAU

Rufaa zilizopokelewa na kushughulikiwa

Katika uteuzi wa wagombea kumekuwa na pingamizi zilizotewa kupinga uteuzi wa baadhi ya wagombea. Pingamizi hizo zilishughulikiwa ngazi ya kata na zilizoshindikana zilikatiwa rufaa kwenye kamati ya rufaa ngazi ya Wilaya. Pingamizi zilizopokelewa na kushughulikiwa ngazi ya rufaa ni kama ifuatavyo:-

Idadi ya Rufaa zilizopokelewa na kushughulikiwa

S/NA.

WILAYA

Rufaa zilizopokelewa

Rufaa zilizoshughulikiwa

1

MVOMERO

2

2

2

KILOSA

9

9

3

ULANGA

18

18

4

KILOMBERO

7

7

5

MOROGORO

2

2

6

GAIRO

0

0

7

MANISPAA

73

73

JUMLA

111

111