Kilimo

Katika sekta ya kilimo, mikakati iliyopo ni  kuboresha na kuharakisha kupatikana kwa hali bora ya uchumi na maisha ya mwananchi kupitia mpango wa Matokeo Makubwa sasa (Big Results Now). Mkoa wa Morogoro una eneo la hekta 2,226,396 linalofaa kwa kilimo kati yake  wastani wa hekta 789,007 sawa na 35.4% ndizo zinazolimwa. Asilimia 76 ya wakazi wa Morogoro hujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, mpunga, migomba, uwele, na mtama kwa ajili ya chakula na mazao ya biashara kama pamba, Ufuta,  alizeti, kahawa, korosho, viungo, mboga na matunda.

Utekelezaji wa FAMOGATA ndani ya KILIMO KWANZA

Utekelezaji wa FAMOGATA ndani ya KILIMO KWANZA unazingatia nguzo kuu kumi za KILIMO KWANZA ambapo Mkoa wa Morogoro uliandaa Mkakati mahsusi mwaka 2009 kama njia mojawapo ya kuanza utekelezaji. Kilimo kinatakiwa kutekelezwa kwa kuzingatia uendelezaji wa kilimo chenye tija kwa kufuata Sera, maelekezo ya Serikali na mikakati inayoongoza ukuaji wa sekta ya uchumi ambayo ni Dira ya Maendeleo 2025, Mini Tiger 2020, Malengo ya Milenia 2010, Mkukuta 2006 – 2010 na FAMOGATA 2007 – 2009.

Utekelezaji wa famogata

Tangu utekelezaji wa FAMOGATA 2006/2007 ulipoanza uzalishaji wa mazao ya chakula umekuwa ukiongezeka kama inavyoonekana katika jedwali hapo chini.

Uzalishaji wa mazao ya chakula  2006/2007 mpaka 2013/2014

Mwaka

Eneo lililo limwa (He)

Uzalishaji

(Tani)

Ziada

(Tani)

2006/2007

344,797.00

957,661.00

444,679.50

2007/2008

368,544.80

885,917.30

372,935.80

2008/2009

404,403.00

1,299,694.00

786,712.50

2009/2010

557,097.00

1,708,963.00

1,195,981.50

2010/2011

598,745.00

2,339,887.50

1,826,906.00

2011/2012

560,955.00

1,369,069.00

842,731.80

2012/2013

594,723.00

1,669,638.00

1,143,300.80

2013/2014

659,660.00

2,210,988.00

1,684,650.80

 Matokeo hayo yanachangiwa na uhamasishaji uliofanywa kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Vijiji na kusababisha kupanua maeneo ya kilimo pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji kama inavyo onekana katika jedwali hapo chini.

Uzalishaji wa zao la Mahindi na Mpunga kuanzia mwaka 2006/2007 mpaka 2013/2014

Mwaka

Eneo lililolimwa (he)

Mahindi

Mpunga

Utekelezaji hekta

Mavuno tani

Tija (tani/he)

Utekelezaji hekta

Mavuno tani

Tija (tani/he)

2006/2007

139,171.00

261,816.00

1.88

106,785.00

226,427.00

2.12

2007/2008

158,884.00

309,012.50

1.94

143,852.00

334,131.00

2.32

2008/2009

155,791.00

319,191.00

2.05

137,108.00

348,729.00

2.54

2009/2010

177,988.00

473,546.00

2.66

170,740.00

479,172.00

2.81

2010/2011

212,753.00

482,116.00

2.27

193,893.00

636,754.50

3.28

2011/2012

223,706.00

372,665.00

1.67

208,153.00

470,601.00

2.26

2012/2013

220,151.00

325,548.00

1.48

242,470.00

780,425.00

3.22

2013/2014

245,780.95

484,147.00

1.97

262,557.50

877,463.00

3.34

  i. Kumekuwa na ongezeko la matumizi ya  zana za kisasa za kilimo kama Matrekta na pawatila.

  ii. Eneo la kilimo cha umwagiliaji maji mashambani kuongezeka kutoka hekta 8,804 za eneo la fursa za umwagiliaji na kufikia hekta 40,558 zinazo mwagiliwa sasa japokuwa lengo lilikuwa kufikia hekta 53,076 mwaka 2010.

Changamoto tulizokumbana nazo wakati wa utekelezaji ni:

Ø Ukosefu wa Rasilimali fedha kutekeleza shughuli za FAMOGATA

Ø Maofisa ugani wachache katika ngazi ya Vijiji

Ø Miundo mbinu duni katika maeneo yenye fursa kubwa ya uzalishaji.

Ø Kuwepo kwa idadi kubwa ya mashamba yaliyo pimwa yasiyozalisha kwa sasa pamoja na maeneo mengine mazuri kwa uzalishaji ambayo hayajapimwa.

Ø Matumizi madogo ya fursa kubwa ya umwagiliaji iliyopo katika mkoa.

Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo mwaka 2013/2014

Katika Msimu wa mwaka 2013/2014 Mkoa ulilenga kulima hekta 819,483 ili kuvuna tani 3, 263,560  za mazao ya chakula na kwa upande wa mazao ya biashara lengo ilikuwa kulima hekta 147,824 ili kuvuna tani 1, 973,260.00 Katika utekelezaji wake mvua za masika zilinyesha vizuri ingawa kulikuwepo na mafuriko kwa baadhi ya maeneo katika Halmashauri zetu. Hekta 659,660.00 zililimwa na kuvuna tani 2, 210,988.00 kwa mazao ya chakula na kwa mazao ya biashara jumla ya hekta 129,341.00  zililimwa na kuvuna tani  2, 062,203.90.

Malengo ya Kilimo mwaka 2014/2015

Katika Msimu wa mwaka 2014/2015 Mkoa umelenga kulima hekta 713,882 ili kuvuna tani 2, 691, 282.00 za mazao ya chakula, na kwa upande wa mazao ya biashara lengo ni kulima hekta 174,887 ili kuvuna tani 3, 183, 072.00.

Pembejeo za Ruzuku.

Pembejeo za ruzuku za kilimo kwa  msimu wa mwaka 2013/2014 zilitolewa kwa  mfumo wa vocha. Mkoa ulipokea na kusambaza jumla ya vocha 195,885 zenye thamani ya Sh. 5, 412, 480,000/= na Mbegu bora zenye ruzuku Tani 10 za alizeti na Tani 5 za mtama  kama ilivyoainishwa katika majedwali hapo chini;-

Mgawanyo wa Vocha kwa ajili ya mazao ya Mahindi na Mpunga

Halmashauri Wilaya/Manispaa

Mbolea

Mbegu za Mahindi

Jumla ya Vocha

Kupandia

Kukuzia

OPV

Chotara

Mpunga

Kilombero

13,000

13,000

8736

3000

1264

39000

Kilosa

10,000

10,000

7039

2000

961

30000

Morogoro

10,000

10,000

7,712

2,000

288

30000

Manispaa ya Morogoro

3,295

3,295

1,500

1,595

200

9885

Gairo

3,000

3,000

2000

1000

0

9000

Ulanga

13,000

13,000

8544

3000

1456

39000

Mvomero

13,000

13,000

7080

5344

576

39000

Jumla (Mkoa)

65,295

65,295

42,611

17,939

4,745

195,885