Elimu

Sekta hii kama ilivyoanishwa kwenye Sera ya elimu ya mwaka 1995, msisitizo umewekwa kwenye elimu ya awali, Msingi  , Sekondari na elimu ya juu.

Mkoa umeongeza idadi ya madarasa ya elimu ya Awali kutoka 326 (2005) hadi 749 (2014) sawa na ongezeko la asilimia 130. Hali kadhalika wanafunzi wa madarasa ya awali wameongezeka toka 22,971 (2005) hadi 43,360 (2014) sawa na ongezeko la asilimia 89. 

Uandikishaji shule za Msingi Mkoa wa Morogro 2014

Na

Halmashauri

Lengo

Utekelezaji

wav

was

jumla

wav

was

jumla

%

1

Kilosa

4,671

4,893

9,564

4,384

4,495

8,879

92.8

2

Manispaa

3,056

3,110

6,166

3,011

3,259

6,270

101.7

3

Mvomero

4,602

4,779

9,381

4,489

4,704

9,193

98.0

4

Ulanga

3,747

3,710

7,457

3,713

3,649

7,362

98.7

5

Kilombero

5,491

5,432

10,923

4,917

5,888

10,805

98.9

6

Gairo

2,490

2,745

5,235

2,393

2,739

5,132

98.0

7

Morogoro(V)

4,622

4,485

9,107

4,339

4,166

8,505

93.4

MKOA

28,679

29,154

57,833

27,246

28,900

56,146

97.1

Chanzo:Taarifa za Wilaya  

Idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka shule 757 (2005) hadi shule 864 (2014) sawa na ongezeko la asilimia 14 na wanafunzi katika shule ya msingi wameongezeka kutoka wanafunzi 379,093 (2005) hadi kufikia wanafunzi 395,616 (2014) sawa na ongezeko la asilimia 4.

Idadi ya walimu katika shule za msingi imeongezeka kutoka walimu 7,965 (2005) hadi kufikia walimu 9,590 (2014), hali hii imepunguza kiwango cha uwiano wa walimu kwa wanafunzi kutoka 1:48 (2005) hadi kufikia 1:41 (2014).

Idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi imeongezeka kwa asilimia 101 kutoka wanafunzi 20,966 (2005) hadi kufikia wanafunzi 42,078 (2014), hali hii imeongezeka idadi ya wanafunzi wanaofaulu kutoka 11,669 (2005) hadi kufikia 21,976 (2013) sawa na ongezeko la wanafunzi kwa asilimia 88.

Hali Walimu Shule Za Msingi Mkoa wa Morogoro 2014

Halmashauri

Idadi ya wanafunzi

Mahitaji ya Walimu

Walimu Waliopo

Upungufu

% Ya Upungufu

Kilombero

76,668

1,917

1,692

225

14

Kilosa

69,737

1,792

1,704

88

05

Morogoro DC

62,680

1,502

1,289

213

14

Morogoro MC

44,015

1,688

1,688

0

0

Ulanga

48,471

1,133

1,037

96

9

Mvomero

58,702

1,540

1,402

138

9

Gairo

35,343

736

478

258

35

Jumla

395,616

10,308

9,590

1,018

10

Kwa upande wa Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi jumla ya wanafunzi 20,966 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2005 ukilinganisha na wanafunzi 42,078 waliofanya mtihani mwaka 2014.Ongezeko hili ni sawa na asilimia 100.69.