Madhumuni ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja
Madhumuni ya mkataba huu ni kufahamisha umma juu ya upatikanaji, aina na viwango vya ubora wa huduma zitolewazo naOfisi ya Mkoa Morogoro, kujenga utamaduni wa kuwafanya watumishi kuwa na mtazamo wa kuwajali wateja, kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja, kuongeza uwajibikaji wa watumishi katika kuwahudumia wateja kwa viwango vilivyowekwa na kutoa mwongozo juu ya taratibu za kufuata endapo huduma zitolewazo na zitakuwa chini ya viwango vilivyowekwa na kukubaliwa. Pia mkataba huu unatoa uwepo wa mfumo wa wazi wa upokeaji wa maoni/ malalamiko na kurudisha mrejesho kwa wateja baada ya kufanyiwa kazi.
Wateja Wetu
Ifuatayo ni orodha ya wateja wanaopokea huduma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro:
Wananchi wote kutoka nje na ndani ya Mkoa, Wizara, Idara za Serikali, Serikali za Mitaa ,Washirika wa Maendeleo; na Umma;
Bodi ya Ushauri ya Wizara (MAB);
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.