• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Kilimo

KILIMO

Mkoa wa Morogoro una eneo la hekta 2,226,396 linalofaa kwa Kilimo ambapo eneo linalolimwa kwa sasa ni wastani wa Hekta 960,034 sawa na asilimia 43. Eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 1,510,339.51 na eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni wastani wa hekta 79,429 sawa na asilimia 5. Mkoa una Skimu za Umwagiliaji 106 (asili na zilizoendelezwa) zinazotambulika zenye ukubwa wa hekta 323,758.15. 

Asilimia 75 ya Wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanategemea kilimo kwa ajili ya Ajira, Kipato na Chakula. Mazao ya Chakula yanayozalishwa kwa wingi ni Mpunga, Mahindi, Ndizi, Viazi vitamu, Muhogo, Mtama na Maharage. Mazao ya biashara yanayozalishwa kwa wingi ni Miwa, Ufuta, Alizeti, Mkonge, Korosho, Pamba, Kokoa, Matunda, Viungo na Mboga mboga.

Idadi ya watumishi (Maafisa Ugani Kilimo) katika Mkoa

Mkoa wa Morogoro una jumla ya Maafisa Ugani Kilimo 462, mahitaji ni 960 na hivyo upungufu ni watumishi 498 kama ilivyo kwenye jedwali namba 20.

Jedwali Na. 1:  Idadi ya Watumishi wa Kilimo Waliopo Kwenye Halmashauri

H/Wilaya

Mahitaji ya Maafisa Ugani Kilimo

Waliopo

Upungufu

Gairo

  55

29

26

Mji Ifakara

78

49

29

Kilosa

184

89

95

Mlimba

81

34

47

Malinyi

65

23

42

Morogoro MC

34

33

1

Morogoro DC

192

73

119

Mvomero

179

102

77

Ulanga

87

26

61

RS Morogoro

5

4

1

Jumla

960

462

498

 

Malengo na Utekelezaji wa Mazao ya Chakula na Biashara

Katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2021/2022, Mkoa ulilenga kulima hekta 940,509.07 ili kuvuna tani 3,035,485.96 za mazao ya chakula. Kwa mazao ya biashara Mkoa ulilenga kulima hekta 205,083.83 ili kuvuna tani 2,704,383.95.

Utekelezaji wake mazao ya chakula, Mkoa ulilima hekta 681,550.68 sawa na asilimia 72 ya lengo na kuvuna tani 1,775,511.71 sawa na asilimia 58 ya lengo. Kwa mazao ya biashara, Mkoa ulilima hekta 155,773.76 sawa na asilimia 76 ya lengo na kuvuna tani 1,743,853.87 sawa na asilimia 64 ya lengo. Kwa msimu wa 2021/2022-unyeshaji wa mvua uliathiri uzalishaji wa mazao kwani Mvua zilianza kwa kuchelewa na hazikunyesha kwa mtawanyiko mzuri na pia ziliwahi kuisha hivyo, kusababisha kutofikia malengo tuliyojiwekea.

Kwa msimu wa mwaka 2022/2023, Mkoa umelenga kulima hekta 938,448.30 ili kuvuna tani 3,068,101.58 za mazao ya chakula na Mazao ya biashara Mkoa umelenga kulima hekta 226,900.73 ili kuvuna tani 2,909,321.78.

Jedwal Na. 2: Mchanganuo wa Eneo Linalofaa kwa Kilimo na Eneo Linalolimwa

Halmashauri

Eneo linalofaa kwa Kilimo 

Eneo linalo lengwa kulimwa kwa sasa

% Eneo faa vs lengwa 

Mazao Makuu 5 yanayolimwa kwa wingi  kwa sasa

  Mazao ya Kipaumbele

Gairo
111,080.4
 100,610.72
91%

Mahindi, Viazi vitamu, Maharage, Alizeti na Mbaazi.

Mahindi na Alizeti.

Ifakara (TC)
131,271.4
46,965.40
36%

Miwa, Mpunga, Mahindi, Ndizi na Muhogo

Mpunga na Miwa.

Kilosa
417,210
262,830.00
63%

Miwa, Mahindi, Mpunga, Viazi Vitamu na Mkonge.

Mkonge na Mpunga.

Malinyi
127,761.06
72,291.70
57%

Mpunga, Mahindi, Ufuta, Korosho na Viazi vitamu.

Korosho, Ufuta/

Mpunga

Manispaa (M)
8,004
6,145.33
77%

Mahindi, Ndizi, Nyanya, Vitunguu na Viungo

Nyanya na Mahindi

Morogoro (DC)
447,000
216,241.50
48%

Mpunga, Ndizi, Mahindi, Muhogo, Ufuta na Viungo

Mpunga na Ufuta/ Viungo

Mlimba
383,884.4
159,850.60
42%

Mpunga, Ndizi, Ufuta, Kokoa na Mahindi

Mpunga na Ufuta/ Kokoa

Mvomero
549,375
202,977.00
37%

Mpunga, Mahindi, Miwa, Maharage na Nyanya.

Mpunga/

Malisho

Ulanga
245,600
97,436.78
40%

Mpunga, Ufuta, Pamba, Kunde na Mahindi.

Korosho na Ufuta/ Karanga Miti

Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri, (2022)

Hali ya Chakula katika Mkoa kwa Msimu wa 2022/2023

Hali ya chakula kwa msimu wa 2022/2023 ni ya wastani katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro kutokana na mavuno ya msimu wa 2021/2022 ambapo Mkoa ulivuna tani 1,775,511.71 sawa na asilimia 58 ya lengo la kuvuna tani 3,035,485.96 ya mazao yote ya chakula. Uzalishaji wa Mazao ya chakula ulishuka kwa asilimia 42 ya lengo kutokana na mvua kuchelewa kuanza, kuwa na kipindi kirefu cha jua na mvua kuisha mapema wakati mazao bado hayajakomaa. Hata hivyo, Halmashauri zote zilivuna Mazao ya chakula kwa utoshelevu hadi ziada.

Jedwal Na. 3:  Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kila Halmashauri 2021/2022

Halmashauri

Malengo

Utekelezaji wa Malengo

Eneo lengwa (ha)

Makisio ya uzalishaji (tani)

Eneo lililolimwa (ha)

% ya lengo la hekta

Uzaliishaji (tani)

% ya uzalishaji

Gairo

79,727.67

218,233.14

61,161.29

77%

84,787.43

39%

Ifakara

39,295.60

180,507.40

32,965.70

84%

86,146.90

48%

Mlimba

135,565.50

419,519.30

121,171.50

89%

385,099.00

92%

Kilosa

191,077.00

579,610.00

111,260.00

58%

265,373.00

46%

Malinyi

73,995.70

219,696.08

61,973.00

84%

132,597.45

60%

Morogoro (DC)

174,547.00

564,142.70

158,870.00

91%

448,819.17

80%

Morogoro (MC)

5,751.16

23,085.62

5,648.88

98%

13,104.84

57%

Mvomero

163,177.00

545,837.00

73,456.00

45%

211,604.00

39%

Ulanga

77,372.44

284,854.72

55,044.31

71%

147,979.93

52%

Mkoa

940,509.07

3,035,485.96

681,550.68

72%

1,775,511.72

58%

Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri, 2022

Aidha, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya watu katika Mkoa wa Morogoro ni 3,197,104. Kutokana na idadi hiyo ya watu mahitaji ya Chakula kwa mwaka 2022/2023 yalikadiriwa kuwa tani 758,512.92 na kufanya Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani 1,016,998.79 bila Mlinganisho wa Nafaka. Kuanzia Mwaka 2014/2015 hadi 2021/2022 Mkoa umekuwa ukijitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ni kama ifuatavyo.

Jedwal Na. 4: Uzalishaji na Mahitaji ya Chakula 2014/2015 Hadi 2021/2022

Mwaka

Eneo lililo limwa (He)

Uzalishaji (Tani)

Mahitaji ya chakula (Tani)

Ziada (Tani)

2014/2015

589,231.00

1,877,942.1

565,779.35

1,312,162.75

2015/2016

563,826.18

1,597,895.65

578,446.05

1,019,449.60

2016/2017

738,282.00

2,298,859.00

591,112.76

1,707,746.24

2017/2018

808,669.00

2,262,227.00

603,779.46

1,658,447.54

2018/2019

784,320.90

2,229,745.92

616,446.16

1,613,299.76

2019/2020

758,568.90

2,016,332.20

629,112.86

1,387,219.34

2020/2021

735,230.97

2,113,776.38

651,573.91

1,462,202.47

2021/2022

681,550.68

1,775,511.71

758,512.92

1,016,998.79

2022/2023
Mkoa umelenga kulima Hekta 938,448.30 ili kuvuna tani, 3,068,101.58 za mazao ya chakula.

Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri za Mkoa wa Morogoro 2014/2015 Hadi 2022/2023

Jedweli Na. 5: Wastani wa Bei za Vyakula Sokoni

Aina ya mazao

Bei (Tsh.) Desemba, 2022

Bei (Tsh.) Januari 2023

Bei (Tsh.) Februari 2023

Gunia la Mahindi (Kg 100)

120,245/=

120,245/=

105,450/=

Gunia la Mpunga (Kg 100)

132,812.50/=-

187,500/=

187,500/=

Unga wa Sembe (Kg 1)

2,000/=

2,000/=

2,000/=

Unga wa Ngano (Kg)

2,000/=

2,000/=

2,000/=

Mchele (Kg 1)

2,800/=-3,400/=

2,800/=3,400/=

2,800/=3,400/

Maharage (Kg 1)

3,000/=

3,200/=

3,200/=-3,400/=

Mkungu wa Ndizi

15,000/=

15,000/=

15,000/=

Viazi mviringo (Kg 1)

1,000/=

1,000/=

1,200/=

Viazi vitamu (Fungu)

2,000-3,000/=

2,000-5,000/=

2,000-5,000/=

 Uzalishaji wa Mazao ya Chakula 2021/2022

Mwenendo wa Mvua na Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo Msimu wa 2022/2023

Mvua za Vuli na Masika msimu wa 2022/2023 zilitabiriwa kuwa za Chini ya Wastani hadi Wastani. Mvua hizo zilitabiriwa kuanza kwa kuchelewa, zenye mtawanyiko usioridhisha na kuambatana na vipindi virefu vya ukavu. Mvua hizo zlinyesha kama ilivyotabiriwa ambapo mvua za vuli zilianza kwa kuchelewa mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022 na hazikua na mtawanyiko mzuri na kuambatana na vipindi virefu vya ukavu (jua) hivyo, kusababisha wakulima wachache kuanza kilimo katika kipindi hicho.

Hata hivyo, kuanzia wiki ya pili ya Mwezi Desemba, 2022 hadi wiki ya tatu Mwezi Januari, 2023 mvua ziliongezeka na kufanya wakulima wengi kuandaa mashamba na kupanda mazao mbalimbali. Hata hivyo, Mwezi Februari hadi mwishoni mwa Mwezi Machi, 2023 mvua ilisimama na kusababisha Mazao yaliyopandwa kunyauka na jua.

Mazao yaliyoathirika zaidi ni nafaka (hasa Mahindi) ambayo yalipandwa kipindi cha mvua za vuli na masika. Halmashauri zinazozalisha mahindi kwa wingi kama Gairo, Kilosa, Morogoro na Mvomero ndizo zimeathirika sana ukilinganisha na Halmashauri zinazozalisha zao la mpunga kwa wingi ambazo ni Mlimba, Malinyi, Ulanga na Ifakara ambapo baada ya Mvua kuanza kunyesha mwezi Aprili Mpunga umeimarika.

Aidha, Eneo lililokuwa limelengwa kulimwa mazao ya chakula ni hekta 938,448.30 ambapo hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2023 eneo lililokuwa limelimwa ni hekta 746,668.26 sawa na asilimia 79 ya lengo na kati ya eneo lililolimwa hekta 225,151.98 sawa na asilimia 30.2 zimeathirika na athari za Ukavu wa muda mrefu.

Jedweli Na. 6: Tathimini ya eneo lililoathirika kwa Mazao ya Chakula katika Halmashauri

Halmashauri

Eneo lengwa (Ha)

Eneo lililolimwa

Eneo lililoathirika (Ha)

Asilimia ya Eneo lililoathirika

Gairo
  79,527.65
55,195.85
23,894.4

43%

Ifakara
  39,295.60
26,322
490.2

2%

Mlimba
148,279.00
143,067.8
32,190.26

22%

Kilosa
190,191.00
162,447
61,442

38%

Malinyi
  69,104.00
66,313
17,241.38

26%

Morogoro (DC)
168,710.00
112,948
28,719.2

25%

Morogoro (MC)
    5,792.16
5,075.61
2,537.8

49%

Mvomero
163,254.00
114,278
53,253.5

46.6%

Ulanga
  74,294.89
61,021
5,383.24

9%

Jumla Mkoa 
938,448.30
746,668.26
225,151.98

30.2

 

Hali ya chakula tarajiwa kwa msimu wa 2022/2023 kutokana na tathmini hiyo, Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro zinatarajiwa kuwa na utoshelevu wa chakula hadi ziada isipokuwa Halmashauri za Gairo, Kilosa na Mvomero zinaweza kuwa na upungufu wa chakula kwa baadhi ya Kata zinazotegemea sana zao la Mahindi kama zao kuu la chakula. Hata hivyo, maeneo mengi Wakulima walishauriwa kufyeka Mahindi yaliyoathirika zaidi na kupanda upya mazao ya muda mfupi pamoja na mazao jamii ya mizizi baada ya Mvua kuanza kunyesha mwezi Aprili.

 Hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Athari za Ukavu wa Muda Mrefu

Halmashauri zilishauriwa kuwanunulia wakulima mbegu za mazao ya muda mfupi na kupandwa kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi na ukame. Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ilinunua jumla ya tani 3 za Mbegu za Mahindi ya muda mfupi (DK 777) na kugawa kwa Wakulima 750 wa Vijiji vya Kata ya Kibati.

Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na matumizi bora ya chakula kwa mazao yatakayovunwa ili kujihakikishia usalama wa chakula kwa Msimu ujao.

Kuhamasisha Wakulima kulima mazao yenye kustahimili ukame na yanayo komaa kwa muda mfupi kama vile Viazi Vitamu, Mihogo, Mikunde, Mtama na Mahindi ya muda mfupi.

Kuwashauri Wakulima wafugaji kupunguza mifugo kwa kuuza na kununua chakula.

Kubaini Maeneo/kaya zilizoathirika zaidi na ukame ili kushirikiana na Wizara ya kilimo kuangalia uwezekano wa Maeneo/kaya hizo kupata mahindi ya chakula kwa bei nafuu kutoka kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa ajili ya kupunguza makali ya bei ya vyakula katika maeneo husika. Ambapo, Mwezi Machi, 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilipokea jumla ya tani 65 za Mahindi ya bei nafuu.

Mahitaji ya Pembejeo za Kilimo

Mbolea 

Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority –TFRA) imeandaa utaratibu wa mfumo wa kielektroniki katika kutoa ruzuku ya mbolea kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa ruzuku, kupunguza mianya ya udanganyifu na gharama za usimamizi. Mfumo huo unatumia programu maalum ya kidigitali kusajili wakulima, wasambazaji/wazalishaji, mawakala pamoja na kuratibu usambazaji wa mbolea kwa wakulima na malipo ya mbolea ya ruzuku.

Utekelezaji wa Rukuzu ya Mbolea katika Mkoa wa Morogoro

Mkoa wa Morogoro umepokea jumla ya Vitabu 3,120 kwa ajili ya kusajili Wakulima ambapo kitabu kimoja kina uwezo wa kusajili (kuandikisha) wakulima 384 hivyo, Mkoa umepokea vitabu vyenye uwezo wa kusajili wakulima 1,198,080. Mkoa umelenga kusajili Wakulima 388,928 ambapo hadi kufikia Aprili 18, 2023, jumla ya wakulima 124,860 walikuwa wamesajiliwa sawa na asilimia 32 ya lengo ambapo kati yao Wakulima 15,752 wamenufaika na Ruzuku ya Mbolea sawa na asilimia 13 ya wakulima waliosajiliwa hata hivyo, usajili wa Wakulima bado unaendelea.

    

Mkoa una jumla ya Makampuni 4 (ETG, Minjingu, TFC na ITRACOM) na mawakala 24 wanaosambaza na kuuza Mbolea kwa Wakulima kwa bei ya Ruzuku isiyozidi shilingi 70,000/= kwa mfuko wa Mbolea wa kilo 50. Vilevile kuna Vyama vya Ushirika 8 vinavyojishughulisha na Kilimo cha miwa katika Bonde la Kilombero ambavyo vinasambaza mbolea. Mahitaji ya mbolea katika Mkoa wa Morogoro kwa msimu wa kilimo 2022/2023 yalikuwa jumla ya tani 27,440.

Hadi kufikia tarehe 18 Aprili, 2023, jumla ya tani 7,976.300 zenye thamani ya shilingi 18,281,872,993 zilinunuliwa kupitia mpango wa Ruzuku kati yake Shilingi 7,522,980,993 ni Mchango wa Serikali (Ruzuku) na Shilingi 10,758,892,000 ni mchango wa Wakulima. Uwepo wa Ruzuku kwenye Mbolea umesababisaha Mahitaji ya Mbolea kuongezeka kutoka tani 27,440 mwaka 2022/2023 hadi tani 36,406 kwa mwaka ujao wa 2023/2024 kama majedwali ya Mahitaji ya Mbolea yanavyoonesha hapo chini.

Jedweli Na. 7: Taarifa ya Matumizi ya Mbolea kwa Mwaka 2021/22 na Makisio ya Mahitaji ya Mbolea kwa Mwaka 2022/23

Halmashauri

Aina ya Mbolea

Matumizi 2021/22 (Tani)

Makadirio ya Mahitaji 2022/23 (Tani)

KILOSA
DAP

600

1,195

UREA

750

1,354

NPK

58

100

CAN

18

20

SA

4

5

Jumla ndogo

1,430

2,674

MALINYI
DAP

5

42

UREA

43

102

NPK

6

16

CAN

16

30

SA

5

30

Jumla ndogo

76

220

MVOMERO
DAP

1,336

2,162

UREA

1,829

3,120

SA

528

1,306

Yara Cereal

15

50

Yara mila winner

12

40

Yara Nitrabor

6

20

Yara sulfan 

12

40

Yara Amidas

45

150

Yara Otesha

15

50

Samadi

131

130

Booster

228

351

Jumla ndogo

4,157

7,419

Gairo
DAP

23

100

UREA

43

100

CAN

17

50

Jumla ndogo

83

250

MOROGORO
DAP

54

1,000

UREA

120

1,000

CAN

96

200

NPK

-

5

YARA CEREAL

55

30

YARA AMIDAS

48

30

Jumla ndogo

373

2,265

MLIMBA
DAP

6

851

UREA

14

1,898

CAN

10

1,265

YARA VELA AMIDAS

32

1,582

Yara Otesha

20

681

SA

14

949

Booster

3

10

YARA CEREAL

3

633

MOP

5

316

Jumla ndogo

108

8,185

MANISPAA
UREA

290

295

DAP

150

215

CAN

70

80

SA

45

45

YARAWINNER

195

YARACEREAL

30

YARAOTESHA

145

OCP

90

SULFANI

45

MOP

10

10

MAGNISIUM

10

10

CALICINITY

30

35

NITRABOR

30

35

AMIGRAN

20

25

AMIDAS

25

KYNOPLAS

10

10

Jumla ndogo

665

1,290

IFAKARA
DAP

115

834

UREA

492

1,050

SA

9

50

CAN

55

100

YARA AMIDAS

35

101

YARA CEREAL

50

99

Jumla ndogo

755

2,234

ULANGA
DAP

210

401

UREA

650

898

CAN

460

665

SA

600

649

NPK

290

290

Jumla ndogo

2,210

2,903

JUMLA KUU

9,857

27,440

Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2021/2022

 

Jedweli Na. 8: Mchanganuo wa Mahitaji ya Mbolea kwa Msimu ujao wa 2023/2024

NA.

HALMASHAURI

AINA YA MBOLEA (TANI)

DAP

UREA

CAN

SA

NPK

MINJINGU

ITRACOM

JUMLA

1.
GAIRO

1,611

2,025

741

565

73

-

-

5,016

2.
IFAKARA

699

6,515

2,764

-

323

285

-

10,586

3.
KILOSA

973

3,676

767

10

151

-

3

5,579

4.
MALINYI

47

127

30

-

-

-

-

204

5.
MANISPAA

447

705

100

15

345

4

-

1,616

6.
MOROGORO

765

765

-

-

20

-

-

1,550

7.
MLIMBA

817

1,597

286

78

155

193

-

3,125

8.
MVOMERO

2,162

4,324

-

1,081

-

33

-

7,600

9.
ULANGA

185

785

75

30

55

-

-

1,130

JUMLA MKOA

7,706

20,520

4,763

1,778

1,121

515

3

36,406

Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2022/2023

Mbegu Bora

Mahitaji ya Mbegu bora za Mazao ya chakula na Biashara ni kama ilivyo kwenye Jedwali lifuatalo hapo Chini.

Jedweli Na. 9: Mahitaji ya Mbegu bora za Mazao kwa Msimu wa 2022/2023

Mbegu bora ya Zao la

Mahitaji ya Mbegu (Tani/Miche)

Mpunga

5,538.88

Mahindi

8,942.21

Ufuta

136.99

Alizeti

320.10

Korosho

Miche 639,275

Mkonge

Miche 52,005,600

Karafuu

Miche 1,480,867

Kokoa

Miche 1,625,312.5

Nyanya

1.5

Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2021/2022

Viuatilifu

Katika msimu wa Kilimo 2022/2023, Mkoa umekabiliwa na uwepo wa visumbufu vya mazao aina ya Panya waharibifu, Viwavijeshi na viwavijeshi vamizi ambavyo vimeshambulia mazao mbalimbali. Mkoa uliomba kiasi cha lita 40,500 aina ya Powercron 720 EC (Profenofos 720g/l) kutoka Wizara ya Kilimo (Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu - TPHPA) ambapo kiasi cha lita 8,400 zilipokelewa katika Halmashauri za Gairo (lita 3,000), Kilosa (lita 1,400) na Morogoro DC (lita 4,000). Aidha, Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo kitengo cha Udhibiti wa panya waharibifu wa Mazao baada ya kupokea taarifa ya Uwepo wa Panya katika Mkoa wa Morogoro walifika katika Halmashauri za Ulanga, Mlimba na Malinyi kwenda Kudhibiti Panya waharibifu wa Mazao.

Kilimo cha Umwagiliaji

Mkoa una eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 1,510,339.51. Eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni wastani wa hekta 79,429 sawa na asilimia 5. Mkoa una Skimu za Umwagiliaji 106 (asili na zilizoendelezwa) zinazotambulika zenye ukubwa wa hekta 323,758.15. 

Miradi ya umwagiliaji inayotekelezwa 2022/2023

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Mkoa unaendelea na utekelezaji wa miradi minne (4) ya Umwagiliaji katika Wilaya tatu (3) kama jedwali linavyoonesha hapo chini.

 

Jedweli Na. 10: Mchanganuo wa Miradi ya Umwagiliaji iliyopata Fedha katika Mkoa wa Morogoro

Wilaya

Mradi

Hatua ya Utekelezaji

Kiasi

Kilosa

Ujenzi wa skimu ya Rudewa

Mradi umefikia 25%. Mkandarasi yuko eneo la kazi na anaendelea na ujenzi.

7,202,268,404.00

Mvomero

Ujenzi wa skimu Kijiji cha Lukenge

Mradi unaendelea na utekelezaji. Mita 1200 kati ya 2750 sawa na 43% zimesakafiwa. Changamoto kubwa ni mahitaji ya pampu ili mradi uweze kutumika.

632,050,865.00

Mvomero

Ukarabati wa skimu ya Mgongola

Mradi umefikia 35%. Mkandarasi yuko eneo la kazi na anaendelea na ujenzi.

5,645,751,182.00

Kilombero

Ukarabati wa skimu ya Idete

Mradi umefikia 13% badala ya 55% iliyotarajiwa. Mkandarasi bado yuko kwenye hatua za awali za utekelezaji. Kasi ya utekelezaji hairidhishi

2,321,015,160.00

JUMLA

15,801,085,611.00

Chanzo: Taarifa za Kilimo Mkoa 2022/2023

Aidha, tarehe 28 Machi, 2023 Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetangaza zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingine minne (4) ambayo mchakato wa manunuzi ya Wakandarasi bado unaendelea. Miradi hii ni Itete uliopo Halmashauri ya Malinyi, Tulo/Kongwa, Kiroka na Mbalangwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Gharama za miradi zitafahamika baada ya mchakato wa manunuzi kukamilika.

Zana za Kilimo

Mkoa wa Morogoro unajumla ya trekta 1,515, trekta ndogo (power tiller) 624 na maksai (majembe ya kukokotwa na wanyamakazi) 16,915 zinazotumika kulima wastani wa hekta 920,680.1. Kati ya hizo, hekta 578,061.80 zinalimwa kwa kutumia trekta, hekta 153,189.90 zinalimwa kwa Maksai, hekta 145,853.00 zinalimwa kwa jembe la mkono na hekta 43,575.40 zinalimwa kwa trekta ndogo. Takwimu hizi zinaashiria mwamko mkubwa kwa wananchi katika matumizi ya trekta katika uandaaji wa mashamba.

Jedweli Na. 11: Mchanganuo wa Zana kwa Halmashauri ni Kama Unavyoonekana Kwenye Jedwali

Na.

H/Wilaya

Matrekta

Powertiller

Maksao

1.

Gairo

42

8

47

2.

Ifakara TC

227

104

816

3.

Kilosa

274

143

1,872

4.

Malinyi

106

42

2,696

5.

Morogoro MC

250

11

5,000

6.

Morogoro DC

153

35

181

7.
Mlimba

174

194

194

8.
Mvomero

239

87

278

9.
Ulanga

50

-

5,831

JUMLA

1,515

624

16,915

Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri 2022/2023

Maghala ya Kuhifadhia Mazao

Mkoa una Jumla ya maghala 842 yenye uwezo wa kuhifadhi Jumla ya tani 476,726.8. Kati ya maghala hayo ya Serikali ni 79 na watu binafsi ni 763.

 

Jedweli Na. 12: Mchanganuo wa Maghala ya Kuhifadhia Mazao katika Halmashauri

Na.

H/Wilaya

Idadi ya Maghala

Uwezo wa Kuhifadhi (Tani)


Gairo

175

13,418


Ifakara TC

151

241,355


Kilosa

111

15,561


Malinyi

59

14,545


Morogoro MC

9

1,825


Morogoro

26

3,921


Mlimba

159

95,087


Mvomero

56

27,080


Ulanga

96

63,934.5

JUMLA

842

476,726.5

Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri 2022/2023

M – Kilimo

M – Kilimo ni mfumo wa kielektroniki unaotoa huduma za ugani na masoko kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi. Lengo la mfumo huu ni kutatua changamoto ya uhaba wa Maafisa Ugani, upatikanaji wa masoko na kuunganisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine katika mnyororo wa thamani. Kwa kutumia mfumo huu, wakulima wanapata fursa ya kuuliza maswali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo na kupata majibu ya hapo kwa papo kutoka kwa Wataalam husika. Ili Mkulima aweze kutumi mfumo anapiga simu na. x152x00#.

Wizara ya Kilimo iliweka lengo la kusajili wakulima 419,776 kwa Mkoa wa Morogoro, mpaka kufikia Januari, 2023, wakulima 445,331 sawa na asilimia 106 ya lengo. Wanunuzi waliosajiliwa ni 1196, wauzaji 1,676 na wataalam wa Kilimo 503.

Kilimo cha Mashamba Makubwa

Katika kuhakikisha lengo la Wizara ya Kilimo la kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikiapo 2030 linafikiwa, moja ya eneo ambalo linatiliwa mkazo ni kuhamsisha kilimo cha Mashamba Makubwa kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kushiriki katika Kilimo. Hili linatekelezwa kupitia mradi wa Jenga Kesho Bora (Building a Better Tomorrow – BBT) ambapo Mkoa utatumia fursa ya mashamba yaliyofutwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan ili kuwawezesha Vijana kupata Ardhi ya Kilimo.

Hadi kufikia Aprili 2023, Mkoa wa Morogoro umepokea jumla ya vijana 124 katika vituo vya mafunzo vitatu; MATI Katrin Vijana 52, Chuo cha Sukari Kilombero vijana 15, MATI Ilonga vijana 57 ambapo wanapata mafunzo ya kilimo biashara katika mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali ya kilimo kabla ya kukabidhiwa ardhi kwa ajili ya kilimo.

Mashamba yaliyofutwa

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mama yetu Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 2021 aliridhia ufutaji wa mashamba kumi na moja (11) yenye ukubwa wa ekari 24,119 yaliyopo katika Wilaya ya kilosa na Mashamba 2 (ekari 11,310) katika Halmashauri ya Mvomero. Aidha, Mhe. Rais aliridhia ugawaji wa mashamba 49 yaliyopo katika vijiji 23 Wilayani Kilosa yenye ukubwa wa ekari 45,788.5 ambayo milki zake zilitwaliwa na kubatilishwa katika vipindi mbalimbali ambayo uhakiki ulibaini sehemu kubwa ya mashamba hayo yanatumiwa na wananchi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji. Wananchi wanaogawiwa sharti wawe wamejiunga kwenye vikundi ili kuondoa tabia ya wananchi kuuza maeneo.

Mazao ya Kimkakati

 

Mazao ya Viungo

Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha mazao ya viungo kwa wingi kama vile karafuu, iliki, mdalasini, vanilla na pilipilimanga. Katika kuendeleza mazao ya viungo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Morogoro wamefanya tathmini ya hali ilivyo kwa kukusanya takwimu za majina ya wakulima wa karafuu, ukubwa wa maeneo yanayolimwa, hali ya uzalishaji, bei, mahitaji ya miche na kubaini maeneo ya wazi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viungo. Jumla ya ekari 84,024 zimebainika kuwa zinafaa kwa kilimo cha mazao ya viungo. Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya ekari 17,219 zimepandwa karafuu, eneo linaloweza kulimwa Karafuu ni ekari 5,931, mdalasini ni ekari 2,263, iliki ni ekari 589 na pilipilimanga ni ekari 1,299. Mahitaji ya miche ya Karafuu ni 1,459,785. Mpaka mwishoni mwa Aprili 2023, Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni Viridium na WWF imetoa miche ya karafuu 27,000 katika Halmashauri ya Morogoro na kusambazwa kwa wakulima bure katika msimu wa 2022/2023.

Zao la Korosho

Mkoa wa Morogoro ni moja kati ya Mikoa inayolima korosho nchini na umeendelea na utekelezaji wa Mpango wa maendeleo ya zao la Korosho katika Halmashauri nane kati ya tisa zilizopo na jumla ya wakulima 1,653 wamesajiliwa na Bodi ya korosho Tanzania kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya wakulima wa zao la Korosho. Halmashauri za Wilaya zinazolima zao la Korosho ni Gairo, Kilosa, Malinyi, Morogoro, Mlimba, Mvomero Ulanga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Ifakara. Mkoa una jumla ekari 36,840 zenye jumla ya Mikorosho 1,550,504.  Kati ya hiyo, mikorosho 408,159 imeanza kuzaa.

Katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 Mkoa ulizalisha jumla ya tani 325.07 za Korosho na kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Mpango/Makadirio ya Uzalishaji Kiwilaya Hadi Kufikia 2025/2026

Mkoa umejipanga kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho kutoka tani 231 hadi kufikia tani 858.5 ifikapo mwaka 2025/2026 kama inavyoonekana katika jedwali.

Jedweli Na. 13: Mpango wa Uzalishaji zao la Korosho kwa miaka mitano ijayo 2021/2022 hadi 2025/2026

S/N
HALMASHAURI

MAKADIRIO YA UZALISHAJI (T)

2021/2022

2022/2023

2023/2024

2024/2025

2025/2026

1
Gairo

5

7

9

13

34

2
Ifakara

2.3

8.6

10.7

24.0

53.5

3
Kilosa

30

45

60

90

120

4
Malinyi

91

108

125

135

150

5
Mlimba

22.5

25.8

55

75

100

6
Morogoro

41

62

91

137

158

7
Mvomero

11

17

25

42

103

8
Ulanga

40

60

85

110

140

Jumla

231.8

333.4

460.7

626

858.5

 

Zao la Pamba

Katika Mkoa wa Morogoro Wilaya zinazozalisha zao la Pamba ni Kilosa, Gairo, Malinyi, Morogoro, Mvomero na Ulanga. Katika msimu wa 2021/2022 jumla ya hekta 2,565 zililimwa na kuzalisha jumla ya tani 1943.49. Pamba yote ilinunuliwa na Bodi ya pamba kwa wastani wa bei ya shilingi 1560 kwa kila Kilo ya Pamba. Katika Msimu wa 2022/2023 Mkoa umelenga kulima hekta 4,357 ili kuvuna tani 3481.20.

Zao la Mkonge

Mkoa wa Morogoro ni Miongoni mwa Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la Mkongo nchini. Halmashauri zinazozalisha Mkonge katika Mkoa wa Morogoro ni Kilosa, Morogoro, Mvomero na Gairo. Hata hivyo, Halmashauri za Gairo na Mvomero hazijaanza kuvuna Mkonge zipo kwenye hatua ya kuhamasisha Wakulima na upandaji wa Mkonge. Maeneo yanayolimwa Mkonge ni wastani wa Hekta 10,573.55 na kuvuna wastani wa tani 12,216.91 kwa mwaka.

Wazalishaji wa Zao la Mkonge Katika Mkoa wa Morogoro

Jedweli Na. 14: Wazalishaji wakubwa na wakati wa zao la Mkonge katika Mkoa wa Morogoro ni kama ifuatavyo

 

Na.

 

Jina la Shamba

 

Mahali lilipo

Ukubwa wa shamba (Hekta)

Eneo lenye Mkonge

Wastani wa Mavuno kwa mwaka


Pangawe Highland Estate
Mkambarani Pangawe – Morogoro vijijini

3,698

1,472.65

2,061.71


FATEMI (Mohamed Enterprises Tanzania Limited)

Kidugalo – Morogoro Vijijini

6,412

3,637

5,819.2


M/S New kimamba Fbres Co. Ltd
Kimamba – kilosa

2,947

2,323.5

1,409


China State Farms Ltd
Rudewa – Kilosa

5,300

2,480

2,573


New Msowero Farm
Msowero – Kilosa

1,360

440

354


Igembe Nsabo - AMCOS
Rudewa – Kilosa

21.4

8.8

0


Josephat Rwezaura
Mkonowamara – Morogoro Vijijini

40

20

0


Mohamed Ramadhani
Mkonowamara – Morogoro Vijijini

80

80

0


Clement Munish ambae
Mkonowamara – Morogoro Vijijini

32

32

0


Wami Sokoine
Mvomero

40

40



Kimambila
Mvomero

11.2

11.2



Vianzi
Mvomero

20

20


 
Gairo
Gairo

8.4

8.4

 

JUMLA

19,970.00

10,573.55

12,216.91

Katika Wilaya ya Kilosa Ipo pia AMCOS ya Lukwambe ambayo imepatiwa na Serikali eneo la kulima Mkonge upandaji unaendelea. Aidha wananchi wanaendelea kugawiwa maeneo ili wajiunge kwenye AMCOS kwa ajili ya kilimo cha Mkonge.

Kilimo cha Kahawa

Zao la Kahawa lilikuwa linalimwa Katika Wilaya za Mvomero, Morogoro Gairo na Ulanga. Aina ya kahawa inayolimwa katika Mkoa wetu ni Robusta na Arabica. Ili kuhakikisha kuwa zao la Kahawa linafufuliwa Mkoa unashirikiana na Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania – TACRI na kutoa elimu ya kuzalisha zao la Kahawa kwa wataalam. TACRI kwa kushirikiana na Halmashauri za Ulanga, Gairo, Mvomero, Morogoro inatoa mbegu na miche kwa wakulima ili kuendeleza zao hilo. Jumla ya kata 28 na wakulima 2,104 wametambuliwa kuwa wakulima wa kahawa Kimkoa.

Ushiriki wa Wadau

Mkoa unashirikiana na wadau mbalimbali kutekeleza programu ya sekata ya kilimo katika Mkoa. Baadhi ya wadau hao ni SAGCOT, USAID, CAU, SAT, MVIWATA, MINJINGU nk.

Mapokezi ya Pikipiki kwa Maafisa Ugani wa Kilimo

Katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha na kuboresha huduma za ugani nchini kwa kugawa vitendea kazi zikiwemo pikipiki, vifaa vya kupima afya ya udongo, vishikwambi na visanduku vya ugani kwa Maafisa Ugani kilimo nchini.

Mpango huu ulizinduliwa na Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 4 Aprili, 2022. Mnamo mwezi Februari, 2023 Mkoa wa Morogoro ulipokea jumla ya pikipiki 436 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo kama ilivyo kwenye mchanganuo ufuatao (Jedwali Na. 23).

Jedweli Na. 15: Mchanganuo wa Maafisa Ugani Kilimo na Mgawanyo wa Pikipiki

Na.

H/Wilaya

Maafisa Waliopo

Wenye Pikipiki kutoka Taasisi za Kilimo/Halmashauri

Pikipiki zilizoletwa na mh Rais


RS Morogoro

4

1

3

1.
Gairo

29

3

26

2.
Mji Ifakara

49

2

52

3.
Kilosa

89

4

87

4.
Mlimba

34

3

34

5.
Malinyi

23

3

20

6.
Morogoro MC

33

6

20

7.
Morogoro DC

73

3

68

8.
Mvomero

102

3

99

9.
Ulanga

26

1

27

Jumla

462

29

436

Pikipiki zote 436 zimefungwa GPS ili kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa ugani katika maeneo yao ya kazi ambapo Afisa ugani anapaswa kuitumia Pikipiki hiyo katika kituo chake cha Kazi na endapo atataka kutoka nayo nje ya Kituo chake cha kazi anapaswa kuomba ruhusa kwa Mkuu wake wa Idara.

Wito kwa Maafisa Ugani wote wa Mkoa wa Morogoro ni kuhakikisha wanazitumia Pikipiki hizo kwa shughuli za Ugani pekee ili kuhakikisha kuwa kilimo katika Mkoa wetu kinaboreshwa zaidi na kuchangia katika uchumi wa Mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.

Changamoto ya Sekta ya Kilimo katika Mkoa wa Morogoro

Upungufu na Ubovu wa Miundombinu ya Umwagiliaji iliyopo, inachangia wakulima wengi kutegemea kilimo cha Mvua ambayo huwa haitabiriki na kusababisha wakulima wengi kushindwa kufikia malengo.

Upungufu wa Watumishi katika Idara za Kilimo, unaokwamisha utendaji kazi kwani baadhi ya maeneo muhimu hasa katika maeneo ya Kata na Vijiji hakuna Wataalam.

Uhaba wa Fedha za Ufuatiliaji, Fedha za usimamizi wa shughuli za Kilimo zinatolewa kidogo sana ukilinganisha na Mahitaji hasa katika ngazi ya Halmashauri.

Baadhi ya Halmashauri kutotoa asilimia 20 ya fedha za Mapato ya Ndani yanayotokana na Kilimo kw ajili ya uendelezaji wa Sekta ya Kilimo (miundombinu ya Umwagiliaji, Mbegu bora, Maghala na WARC) kitendo hicho kinachangia Sekta ya Kilimo kuonekana siyo kipaumbele wakati ndio inategemewa katika ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri hizo.

Kutokuwa na Mafunzo Rejea (On Job Training) kwa Wataalam wa Kilimo hivyo, kusababisha baadhi ya Wataalam kutoendana na teknolojia za kisasa hivyo, kulalamikiwa na Wananchi.

Mikopo kwa Wakulima, taasisi za mkopo (Mabenki) kuwa na masharti yasiyorafiki kwa Wakulima hivyo, kusababisha Wakulima kuendelea kunyonywa na Madalali ambao Wakati wa Kulima na Palizi kipindi ambacho wakulima hawana hela wanakopeshwa fedha na madalali kwa kigezo kuwa Mkulima akivuna mazao atamlipa Mazao badala ya fedha hasa kwa zao la mpunga.

Kutokuwa na bei ya kueleweka ya mazao ya Nafaka (Kupanda na kushuka kwa bei bila mpangilio) Price fluctuation. Kunasababisha wakulima kushindwa kupanga bei ya mazao ili wapate faida.

Maeneo ya kuhifadhia mazao (Maghala) ni machache hivyo, kusababisha wakulima kuuza bila mpangilio.

Uingizaji wa Mbegu za mazao za Nafaka kutoka nje ya nchi kunachangia kupotea kwa mbegu nzuri za asili.

Baadhi ya mawakala waliosajiliwa kupitia mfumo wa Mbolea ya Ruzuku kupitia TFRA kutokuwa na uwezo wa kimtaji wa kuuza mbolea kusababisha wakulima wengi kufuata mbolea kwa umbali mrefu maeneo ya Mjini na kuona kuwa ni kero.

Namna ya kutatua baadhi ya changamoto hizo ni kama ifuatavyo;

Kuimarisha AMCOS kwa ili wakulima waweze kuhifadhi mazao kwa pamoja na kutafuta masoko ili kuuza mazao kwa bei nzuri.

Kuimarisha Miundombinu ya Kuhifadhia mazao (Maghala) ambapo Halmashauri zimeshauriwa kutumia mapato ya ndani (asilimia 20 ya mapato yanayotokana na kilimo) kujenga maghala angalau kila Kata kuwe na ghala na vifaa vyote muhimu vinavyo hitajika ikiwemo kipima unyevu (Moisture meter) ili wakulima waweze kuhifadhi mazao na kuuza kwa pamoja.

Kutumia fursa ya Mhe. Rais kutoendeshwa na Wahisani (Donors) kwa kupigania Sera zetu badala ya kufuata wanachotaka wao.

Kutozuia mazao ya Chakula kuuzwa nje ya Mkoa na nje ya nchi ili wakulima kuuza kwa faida.

Kuwe na vituo maalum vya kuuzia Nafaka kwa kila Kijiji/Kata ili kudhibiti Madalali na ubora wa mazao ya Nafaka.

Kutoa elimu kwa wakulima ili wauze mazao yao kwa njia ya Minada ya Soko la bidhaa (TMX) badala ya kuuza mmoja mmoja.

Kuainisha Vituo vya Kuuzia Mbolea kulingana na Mahitaji ili Msimu wa Kilimo wa 2023/2024 Wakulima wapelekewe Mbolea katika Maeneo yao.

Pamoja na changamoto hizo, tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa Vitendea kazi (Pikipiki) kwa Maafisa Ugani Kilimo na Ruzuku ya Mbolea kwa Wakulima, kwani mwamko umekuwa mkubwa sana Wakulima wengi wamelima mazao mbalimbali kutokana na kupunguziwa bei ya Mbolea pia Wataalam wanawafikia Wakulima kwa urahisi kutatua changamoto zao.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Zaidi ya Mil. 125 zachangwa kupitia chakula cha hisani kukarabati Hospitali ya Rufaa Morogoro.

    May 18, 2025
  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.