• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Jamii yatakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa.

Posted on: August 19th, 2022

Jamii yatakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu wakati wa Sensa

Kuelekea zoezi la sensa ya watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu, jamii imeaswa kutowaficha watu wenye ulemavu badala yake wawawezeshe kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu sahihi za kundi hilo kwa faida yao na taifa kwa jumla.

Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Morogoro Bi. Margareth Mkanga.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Morogoro Bi. Margareth  Mkanga Agosti 18, 2022 wakati akifunga kikao cha wajumbe wa kamati hiyo  kilichofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Wajumbe wa kamati ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Morogoro.

Bi. Mkanga amewataka wazazi ama walezi wa watu wenye ulemavu wakishirikiana na wenyeviti wa Mitaa ama vitongoji kutowaficha watu wenye ulemavu ifikapo Agosti 23 mwaka huu ili Serikali kupata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu zitakazosaidia mipango yake lakini pia takwimu hizo zitasaidia utekelezaji wa mipango ya Kamati hiyo waliojiwekea.



“nasisitiza suala la watu wenye ulemavu wasifichwe na hizo familia husika au na hao wenyeviti wa mitaa husika” amesema Bi. Mkanga

“...lakini pia hapa ndipo itakaposaidia action plan yetu ili tujue exctly tuna watu wenye ulemavu wangapi Mkoa huu na wa aina zipi” amesisitiza Mwenyekiti huyo.

Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Bi.Jesca Kagunila

Akitoa taarifa ya Mkoa kuhusu watu wenye ulemavu, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bi. Jesca Kagunila amesema Mkoa wa Morogoro kwa mwaka wa fedha 2021/2022 wametambua jumla ya watu wazima wenye ulemavu 11,415 na watoto wenye ulemavu 3,298.

Aidha, amesema jumla ya watu wenye ulemavu 1,374 wamepewa huduma mbalimbali huduma zilizolenga kutoa hamasa kujiunga na vikundi ili waweze kufaidika na asilimia 2 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri.

Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro akitoa taarifa ya hali halisi ya watu wenye ulemavu Mkoa wa Morogoro.

Mbali na huduma hizo huduma nyingine zilizotolewa kwa watu wenye ulemavu kwa mwaka 2021/2022 ni pamoja na wengine kupatiwa msaada wa kisaikolojia, vifaa saidizi pamoja na watu wenye ulemavu 190 kupewa misamaha ya matibabu au matibabu bila malipo.

Wajumbe wa Kamati ya watu wenye ulemavu wakiwa kwenye kikao.

Aidha, Bi. Jesca amebainisha huduma nyingine walizopewa watu wenye ulemavu kuwa ni pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi 237 kupewa huduma ya Afya ya ngozi na kufanyiwa uchunguzi zaidi kwa jitihada za Serikali ngazi ya Mkoa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Standing Voice, huku watu wenye ulemavu 347 wampewa huduma ya macho kwa kushirikiana na shirika la sight savers. 


Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoa wa Morogoro Oscsar Changala ametoa onyo kwa vijana wanaowatumia watu wenye ulemavu kama kitega uchumi kwa kuzunguka nao mitaani kuomba fedha kuacha tabia hiyo mara moja na kwamba kuanzia sasa watakaokaidi onyo hilo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.

 “Kwa hiyo nawaeleza wazi kwa watu wanaofanya hiyo bishara kila mtu aanze kutafuta pori” ameonya Mwenyekiti huyo

 

MWISHO 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.