• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Miradi 67 ya maji kutekelezwa Morogoro.

Posted on: January 15th, 2021

Shilingi Bilioni 9.3 zimetengwa Mkoani Morogro kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji 67 ambayo ipo vijijini na itatekelezwa ndani ya mwaka wa fedha 2020/2021.

Hayo yamebainisha Januari  15 mwaka huu na Mkurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi John Msengi katika kikao kazi cha wadau wa maji Mkoani Morogoro kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Morogoro Hotel.

Mkurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi John Msengi akisikiliza maoni ya wadau kuhusiana na Kikao hicho.

Mhandisi Msengi amebainisha kuwa hadi Disemba 2020 huduma ya maji katika Mkoa wa Morogoro ilifikia asilimia 69 Vijijini na maeneo ya Mijini asilima 81ambapo lengo kubwa la kikao hicho lilikuwa ni kushirikishana  mipango  katika kuhakikisha huduma ya maji katika Mkoa huo inafikia asilimia 85 Vijijini na  asilimia 95 Mijini kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi – CCM ya mwaka 2020/2025.

 Aidha, Mhandisi Msengi amesema katika miradi hiyo 67 inayotarajiwa kutekelezwa Mkoani humo italeta mapinduzi katika sekta ya maji ambapo atashirikiana na Wahe. Wabunge kuhakikisha  kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama ndani ya miaka mitatu ijayo.


Baadhi ya Wakuu wa Wilaya walioshirikiki katika Kikao kazi cha wadau wa maji Mkoani Morogoro, wa kwanza ni  Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi, wa pili ni Siriel Mchembe Mkuu wa Wilaya ya Gairo

Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maji, Mhandisi Msangi amesema kutokuwepo kwa fedha za kutosha kukidhi gharama za uendeshaji wa miradi hiyo na uharibifu wa vyanzo vya maji unaopelekea vyanzo hivyo kukauka ni changamoto kubwa inayojitokeza katika Mkoa huo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, amesema hali ya upatikanaji maji safi na salama Mkoani humo  kwa takwimu za  Disemba 2020 kuna ongezeko la  asilimia 13 kutoka asilimia 56 kwa mwaka 2015 ambapo kwa Manispaa ya Morogoro  upatikanaji wa maji hayo imefika asilimia 81.

Wabunge kutoka Majimbo tofauti Mkoani Morogoro ambao wamehudhuria kikao kazi cha maji Mkoani Morogoro, kushoto ni Mhe. Abubar Asenga (Kilombero) kushoto kwake ni Mhe. Dennis Londo (Mikumi), anayefuata ni Mhe. Innocent Kalogelesi (Morogoro Kusaini) na Mhe. Tale Tale  (Morogoro  Kusini Mashariki)

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wahe, Wabunge kutoka Mkoani Morogoro akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakar Asenga amesema jimbo lake linakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji kutokana na jimbo hilo kuongezewa kata kumi hivyo kufikia jumla ya kata 19.

Pia, amesema katika Jimbo lake kuna mradi wa maji mserereko  wa zaidi ya shilingi bilioni sita ambao unatarajiwa kuhudumia  wananchi 125,000 kutokana na takwimu za mwaka 2020.

Naye, Mbunge wa Jimbo la Mikumi Denis Londo, amesema licha ya maji kuwa changammoto katika Jimbo lake kuna mradi wa maji wa Madibila ambao ushafanyiwa kazi, kilichobaki ni kupata fedha zitakazowezesha  kupata maji ya mserereko kutoka chanzo hicho ambacho kitaondoa changamoto ya maji katika Tarafa ya Mikumi.

Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya  Wilaya ya kilosa Ndg. Amer Mubarak amesema kuna mwingiliano mkubwa wa kazi baina ya MORUWASA na RUWASA hali inayopelekea mamlaka hizo kushindwa kutekeleza wajibu wao inavyotakiwa, hivyo ameiomba Serikali iingilie Kati kutatua changamoto hiyo.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.