• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAIAGIZA ASA KUSAFISHA MASHAMBA.

Posted on: February 18th, 2025


Kamati ya Kudumu ya bunge  viwanda, biashara, kilimo na mifugo chini ya mwenyekiti wake Mhe. Deo Mwanyika (MB) imeiagiza  Wakala wa  Uzalishaji  na Usambazaji wa mbegu nchini (ASA) kusafisha mashamba ya  kuzalisha mbegu ambayo kwa sasa ni mapori ili yaweze kutumika na  kusaidia  kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu na kukidhi mahitaji ya wakulima.

Agizo hilo limetolewa  Februari 18, 2025 na Mhe. Mwanyika ambaye ni mwenyekiti wa Ka ati hiyo ya kudumu wakati wa ziara ya  kutembelea Kituo cha ASA kilichopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Mhe. Mwanyika amesema, kutokana na kuwepo kwa   uhitaji  mkubwa wa   mbegu hapa  nchini ameitaka ASA kufufua mashamba ambayo yalikuwa yanatumika katika uzalishaji wa mbegu  ambayo yatasaidia katika uzalishaji wa mbegu na  kupunguza  uhitaji wa serikali kuagiza   mbegu  kutoka nje ya nchi.

"..Hatutaki kuona mashamba ya mbegu ambayo ni mapori" Amesisitiza Mhe. Deo Mwanyika.

Aidha kiongozi huyo ameitaka ASA kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uzalishaji yakiwemo matrekta na vifaa vingine ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kuleta faida kwa taifa la leo na hata la kizazi kijacho.

Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo Mhe. David Silinde  amesema  Serikali  inafanya jitihada ya kuhakikisha uzalishaji   wa mbegu unaongezeka ili kupunguza changamoto ya uhaba wa mbegu kwa wananchi ambapo kwa sasa mbegu zinaagizwa kutoka nje ya nchi hivyo amezitaka taasisi za uzalishaji mbegu na usambazaji kuongeza uzalishaji wa mbegu hizo hapa nchini.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima  amekitaka kituo cha utafiti wa Mbegu Tanzania (TARI) kuendelea kufanya Tafiti mbalimbali za uzalishaji wa mbegu ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mbegu katika maeneo mengi na kukidhi uhitaji wa mbegu kwa watanzania wote.

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge viwanda, biashara, kilimo na mifugo itendelea na ziara yake Februari 19,2025 katika Halmashauri ya Mji ifakara.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.