• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI AAGIZA USIMAMIZI WA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI.

Posted on: March 26th, 2023

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akizungumza na washiriki wa mafunzo ya stakabadhi ghalani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewaagiza bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala kwa kushirikiana na wadau wengine hapa nchini kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ili Umma upate uelewa na kufanya maamuzi juu ya namna ya kuendesha mfumo huo.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli kwenye ufunguzi wa mafunzo ya stakabadhi ghalani.

Dkt. Hashil ametoa agizo hilo Machi 24, 2023 wakati akizindua matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani wa zao la iliki pamoja na mafunzo kwa makatibu tawala wasaidizi wa mikoa Uchumi na Uzalishaji yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biahara Dkt. Ashatu Kijaji, Katibu huyo amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya ufahamu wa kutosha kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani kwa wakulima ili kuimarisha Ushirikiano, uwazi na uwajibikaji na lengo kuu likiwa kuimarisha na kulinda mfumo huo usihujumiwe.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akizindua ghala la kuhifadhia nafaka Wilayani Mvomero.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akikagua mfumo wa stakabadhi ghalani namna unavyofanya kazi.

Aidha amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi katika kueleza faida za mfumo huo, na kusimamia mfumo huo ili  uwanufaishe  wakulima huku akisisitiza utaratibu mzuri wa kusimamia  mkulima kupata haki yake ya malipo badala ya mkulima kusubiri malipo kwa muda mrefu kwani hiyo itapelekea wakulima kuuchukia mfumo huo.

“Mnatakiwa kulinda, kuthamini na kuheshimu haki za wakulima kwa ili kuondoa malalamiko miongoni wakulima.  Hatutavumilia kitendo cha kuwanyanyasa wakulima haki zao ndani ya muda unaostahili”.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amesema kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani, Halamashauri hiyo imeongeza uwezo wa makusanyo ya mapato kutoka Shillingi milioni nane hadi Shilingi milioni 148.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli akizungumza na washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya ya stakabadhi ghalani.

Ameongeza kuwa, Mfumo wa stakabadhi ghalani una faida  sio kwa Serikali pekee katika kukusanya mapato lakini pia kwa wakulima kwa kupata bei nzuri  na shindani, kwa kuwa mfumo umemuwezesha mkulima kuuza pasipo kutumia dalali hivyo kutonyonywa haki yake.

Pamoja na kuahidi kusimamia Mfumo wa stakabadhi gharani Wilayani humo Mkuu huyo wa Wilaya amesema amewataka wakulima wa Wilaya ya Mvomero kulima iliki kwa wingi kwa kuwa ardhi na hali ya hewa Wilayani humo ni rafiki kwa zao hilo ambalo litawaletea tija kwao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Yusuph Makunja amesema yeye na wananchi wake wanaamini kuwa watakuwa salama zaidi katika kilimo kama watatumia mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuwa mfumo huo maana yake ni kutafuta soko la yaani wanunuzi wengi watakaoshindani kununua mazao yao hivyo kuuza kwa tija.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa stakabadhi ghalahi wakimsikiliza mgeni rasmi.

Akifunga Mafunzo hayo ya Siku moja Katibu Tawala Msaidizi Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bi. Beatrice Njau kwa Niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kwanza kushirikiana katika kufanya kazi zao lakini pia wasimamie kikamilifu mfumo wa stakabadhi ghalani Uweze kufahamika kwa wakulima na mwisho kuimarika na wafanye hayo kwa kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu za Serikali lengo ni kuleta tija kwa wakulima.

Katibu Tawala Msaidizi Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bi. Beatrice Njau akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa stakabadhi ghalani.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.