• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

KAZI YANGU YA KWANZA NI KUHAKIKISHA KUWA MOROGORO INAKUWA NA MISINGI YA AMANI - MHE. ADAM MALIMA, RC MORORORO

Posted on: May 27th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema kazi yake ya kwanza kama Mkuu wa Mkoa huo ni kuhakikisha kuwa kuna Amani na Utulivu ndani ya Mkoa huo kwa ajili ya wanamorogoro pamoja na wawekezaji wanaotamani kuja kuwekeza ndani ya Mkoa huo.

Mhe. Kigoma Malima amesema hayo Mei 26, 2023 wakati wa kikao cha kujitambulisha kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa huo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya kikao na wajumbe hao tangu alipoteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wiki moja iliyopita kushika nafasi hiyo.

Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa kwenye kikao cha kujitambilisha.

Amesema, jukumu lake la kwanza kama Mkuu wa Mkoa ni kulinda Amani na Utulivu viwepo hivyo wananchi kuendelea kufanya kazi zao za uzalishaji mali kwa Amani na utulivu lakini pia Amani hiyo itawezesha wawekezaji kuvutiwa kuja kuwekeza ndani ya Mkoa wa Morogoro

“Kwa hiyo, kazi yangu ya kwanza ni kuhakikisha kwamba Morogoro ina misingi ya AMANI na UTULIVU inayoongoza wananchi kufanya kazi zao ” amebainisha Mhe. Adam Malima.

Aidha, amesema jukumu lake la pili ni kusimamia maendeleo ya wananchi wa Morogoro na ya Serikali kwa ujumla kwa kuangalia na kushauri utekelezaji wa miradi hiyo ya Serikali inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo.

Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wakimsikiliza Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo, amesema ili kutekeleza majukumu hayo makubwa ushirikiano unahitajika, kwa kuwa peke yake hawezi kukamilisha azma hizo za Mkoa na Serikali ya awamu ya sita, isipokuwa ni kwa kufanya kazi kama timu.

Kwa sababu hiyo, amewataka Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa huo kumpa ushirikiano  unaohitajika ili aweze kutekeleza majukumu hayo na mengine kwa kuwa peke yake hawezi kufanikiwa.

Akisisitiza suala la ushirikiano amesema kwenye suala la Amani, Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama watatakiwa kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kudumisha  Amani ya Mkoa huo na kwa upande wa usimamiaji wa miradi ya maendeleo Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa na wanatakiwa kuwajibika kutoa ushirikano huo kwake.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ali Mussa amewataka wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa huo kubadilika na kufanya kazi kulingana na wakati na mazingira yaliyopo badala ya kuendeleoa kufanya kazi kwa mazoea.

Aidha, amewataka Wajumbe hao kuwa na desturi ya kuwasiliana baina ya idara moja na idara nyingine katika utekelezaji wa majukumu yao jambo ambalo amesema bado ni changamoto katika taasisi hiyo.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.