• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

LISHE BORA NI HAKI YA KILA MTOTO, SOTE TUWAJIBIKE

Posted on: August 8th, 2022

Lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  lakini mara nyingi watoto hukosa  lishe bora kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo hali ya kipato, kutokuwa na elimu sahihi kuhusu Lishe bora pamoja na mila na desturi za jamii.


Amesema hayo agosti 8, 2022 katika kikao cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.


"udumavu huu wa akili hupelekea mamilioni ya watoto kuwa na tatizo la akili na kusababisha tatizo kwa jamii nzima... tunatakiwa kutoa elimu ya Lishe bora, kwani ni haki ya Msingi kwa kila mtoto kwa maendeleo ya jamii..." amesema Mhe. Fatma Mwassa


Mhe. Mwassa amesema hali hiyo  inaweka afya za watoto hatarini kwani hupelekea tatizo la udumavu wa akili na kujenga jamii yenye tatizo la Afya ya akili, na utapiamlo kwa kukosa lishe bora, lakini wengine hata hushindwa kuhudhuria masomo katika shule zao.


Nae Bi. Salome Magembe, Afisa Lishe Mkoa wa Morogoro amesema  kuna idadi kubwa ya watoto wenye udumavu ambapo utafiti uliofanyika mwaka 2018 ulionesha 26.4% sawa na watoto 100,730 wana udumavu kwani hali hiyo hupunguza nguvu kazi kimwili na kiakili na kuchochea changamoto za uzalishaji katika Taifa. 


Sambamba na hilo, Bi. Salome amesema mikakati iliyowekwa katika kikao hicho ni kutoa elimu ya lishe kwa jamii kupitia viongozi mbalimbali wakiwemo maafisa watendaji wa Kata na maafisa Lishe waliopo katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro.


Kwa upande wake, Bw. Simon Mkali Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mlimba, Mkoani Morogoro amesema mila na desturi ni changamoto kubwa kwa jamii hizo kwani wazazi hushindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo, sambamba na hilo amesema kuwa wanajukumu kubwa la kuelimisha jamii ili kujenga jamii yenye uelewa kuhusu Lishe bora.


Mwisho.


Matangazo

  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro April 13, 2023
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • View All

Habari Mpya

  • RAS Morogoro awataka Viongozi waSerikali kujitathmini utekelezaji wa mkataba wa Lishe.

    June 03, 2023
  • RC MOROGORO AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI MUELEKEO WA MKOA.

    June 02, 2023
  • RC MALIMA AKABIDHIWA OFISI RASMI, AAHIDI KUWEKA MIKAKATI KUUENDELEZA MKOA HUO.

    June 01, 2023
  • RAS Morogoro afunga rasmi UMITASHUMTA, atoa agizo kwa wakurugenzi

    May 30, 2023
  • View All

Video

Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.