• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MKAKATI WA LISHE BORA NI SEHEMU YA MALENGO YA SERIKALI KUELEKEA KWENYE MAPINDUZI YA VIWANDA

Posted on: February 15th, 2022

MKAKATI WA LISHE BORA NI SEHEMU YA MALENGO YA SERIKALI KUELEKEA KWENYE MAPINDUZI YA VIWANDA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge amesema mkakati wa lishe bora hapa nchini ni moja ya malengo ya Serikali kuelekea kwenye mapinduzi ya viwanda na maendeleo ya nchi kwa kuwa ubora wa mtu kiakili katika kuleta mapinduzi unategemea siku 1000 tangu mama kutungwa mimba.

Aboukar kunenge amesema hayo Februari 15 mwaka huu wakati akifungua mkutano wa nusu mwaka wa tathmini ya Mkataba wa lishe na Bima ya Afya ya Jamii iCHF uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa CCT uliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Aboubakar Kunenge ambaye kwa sasa ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema, ili nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele ni muhimu kutilia mkazo suala la Lishe Bora hususan malezi ya mtoto ndani ya siku 1000 tangu mama kutungwa mimba kipindi ambacho hupelekea ubora unaohitajika kwa mtoto atakayezaliwa  na hivyo kuweza kuleta maendeleo katika nchi.

“Kwa hiyo lazima tuhakikishe mkakati wa kuinyanyua nchi yetu…. ni aina ya watu kwa sababu ‘what matters most’ katika resources za aina yoyote tulizo nazo ni Rasilimali Watu. Na ubora wa Rasilimali Watu kwa mujibu wa Sayansi ni siku 1000 za kwanza” amesema RC Kunenge.

Kwa sababu hiyo, Mhe. Kunenge amewataka viongozi wa Mkoa wa Morogoro na watumishi wote wa umma kutekeleza mkataba wa Lishe huku akiwataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kutosa fedha zinazohitajika kutekeleza mkataba huo bila kusukumwa na mtu kwa kuwa kila mtendaji atapimwa utendaji wake kutokana na namna alivyotekeleza Mkataba huo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi na watumishi wote wa Serikali Mkoani humo kusimamia kwa dhati zoezi la Anwani za Makazi, huku akibainisha kuwa zoezi hilo lina umuhimu kwa zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi sio geni  hapa nchini, limekuwa likifanyika kila baada ya miaka kumi, hata hivyo zoezi hilo kimsingi limekuwa linafanyika upande mmoja wa Sensa ya watu pekee huku suala la makazi likiachwa na kwamba mwaka huu itakuwa ni mara ya kwanza zoezi la Makazi kufanyika, hivyo ufanisi wa Sensa ya watu ya mwaka huu inategemea sana utekelezaji wa zoezi la anwani za Makazi ambalo linatakiwa kukamilika kabla au ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Kwa sababu hiyo, amewakumbusha watendaji kutekeleza zoezi la anwani za Makazi kwa mujibu wa maelekezo ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kwanza kulifanya zoezi hilo kama operesheni, pili Wakurugenzi kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hilo lakini pia kuwa waadilifu dhidi ya fedha za zoezi hilo na kamwe fedha hizo zisitumike kama posho.

Akizungumzia zoezi la chanjo ya UVIKO – 19, Mkuu wa Mkoa Aboubakar Kunenge ameagiza kila mmoja kujiwekea mikakati ya kuhamasisha zoezi la chanjo kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wengine, huku akibainisha kuwa itakuwa aibu na fedhea kubwa kwa Tanzania endapo dawa hizo za chanjo zitaharibika (expire) wakati watanzania wako katika changamoto ya kupoteza maisha kutokana na ugonjwa ambao dawa zake zinaharibika.

Kwa upande wake Mratibu wa huduma za chanjo Mkoa wa Morogoro Dkt. Masumbuko Igembya amesema walengwa wa chanjo ya UVIKO – 19 Mkoa wa Morogoro hiyo ni 1,759,666 na waliochanja hadi Februari 15, 2022 ni  watu 150,326 pekee sawa na 9% tu ya wakazi wa Mkoa wa Morogoro ukilinganisha na lengo la 60% la wakazi hao ambao wana sifa ya kuchanjwa.

Hata hivyo, amesema idadi ya wagonjwa wenye maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO – 19 katika Mkoa huo imepungua na wagonjwa ambao wanafika katika vituo vya kutolea huduma za afya na kugundulika kuwa na ugonjwa huo hususan wanaofikia hatua ya kulazwa na kuwa na hali mbaya ni wale ambao hawajapata chonjo ya UVIKO -19.

Hata hivyo Dkt. Masumbuko amesema changamoto kubwa inayowakabili katika zoezi la chanjo ni idadi ndogo ya watu wanaostahili  kupata chanjo mara ya pili kushindwa kumalizia dozi ya pili, huku akibainisha kuwa hadi sasa wlengwa 20,000 ambao wamestahili kupanta chanjo mara ya pili wameshindwa kurudi na kumalizia dozi ya pili. Amesema hali hiyo inaashiria kwamba wateja hao hawana kinga kamili ya UVIKO 19 na kutoa wito kwao kurudi kukamilisha dozi hiyo ili kujihakikishia kinga kamili ya ugonjwa huo.

Naye mratibu wa iCHF Mkoa wa Morogoro Elisia Mtesigwa amesema lengo la Mkoa huo kwa mwaka 2021/2022 ilikuwa kuandikisha kaya 50,600 katika bima hiyo lakini hadi kufikia Februari 15, mwaka huu walikuwa wameandikisha kaya 8,900 pekee jambo ambalo amekiri kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Hata hivyo Mtesigwa ameendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya iCHF kwa kuwa una gharama ndogo ya matibabu ambapo mchango wa shilingi 30,000/= unaotolewa na mwanachama una uwezo wa kutoa matibabu kwa watu sita kwa mwaka mzima tena mahali popote atakapokuwepo ndani ya Tanzania.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.