Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Bin Zuber amewataka Viongozi wa ngazi zote za dini hiyo hapa nchini kutumia mawaidha wanayotoa katika misikiti yao na maeneo mengine yalenge kuwaelimisha waumini wao kulinda maadili na tabia njema huku wakikemea maadili yasiyofaa ili kulinda kizazi hiki na kizazi kijacho.
Sheikh Abubakari amesema hayo Mei 18, 2024 wakati akizungumza na Viongozi wa BAKWATA Mkoani Morogoro wakiwemo Mashekhe, Maimamu na Wajumbe wa Baraza katika msikiti wa Masjid Boma road ikiwa ni ziara yake ya siku 2 Mkoani humo iliyoanzia Mei 17 hadi 18, 2024.
Sheikh Abubakari alitarajiwa kuondoka Leo Mei 19, 2024 Mkoani hapa kurudi Jijini Dar es Salaam baada ya kukamilisha ziara hiyo.
Mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.