• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mwenge wa Uhuru waagiza jeshi la polisi Morogoro

Posted on: August 31st, 2022

JESHI LA POLISI MOROGORO KUFANYA MSAKO WA BANGI

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limeagizwa kufanya msako wa mara kwa mara na kufichua biashara ya Bangi inayoendeshwa Mkoani humo ili kuhakikisha vijana wa wa Mkoa huo na watanzania wengine hapa nchini wanabaki salama na kujikita suala nzima la maendeleo ya ujenzi wa Taifa lao.

Agizo hilo limetolewa leo Agosti 31, 2022 na mmoja wa Wakimbiza Mwenge wa kitaifa kwa niaba ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Geraruma wakati akitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya Msingi Lupilo Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro.

Ili kukomesha tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya hususan bangi Kiongozi huyo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Morogoro ambao ni mmoja wa mikoa yenye changamoto ya wananchi wachache wanaojihusisha na kilimo haramu cha bangi kufanya msako wa mara kwa mara wa biashara hiyo kwenye maeneo ambayo inafanyika.

“mwenge wetu wa uhuru unaagiza vyombo vya dola hususan jeshi la polisi kufanya msako wa mara kwa mara kwenye maeneo niliyoyataja na maeneo mengine yote yanayoendesha kilimo cha bangi ndani ya Mkoa huu wa Morogoro” ameagiza.

Akibainisha zaidi juu ya mapambano ya madawa ya kulevya chini ya kaulimbiu isemayo “tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya tuokoe maisha” Kiongozi huyo kwa niaba ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa amesema vijana wanapotumia madawa ya kulevya hupoteza dira, mwelekeo pamoja na ndoto zao hivyo mwenge huo umewataka vijana kuachana kabisa na matumizi ya dawa hizo hususan Bangi.

Aidha, Mkimbiza mwenge huyo  amebainisha maeneo ambayo vijana wengi wamekuwa wakiyatumia kwa ajili ya bishara hiyo ya bangi kuwa ni pamoja na  fukwe za bahari, kumbi za starehe, nyumba za kaya maskini na majumba yaliyotelekezwa na kuitaka jamii kupinga biashara hiyo kwa maslahi mapana ya jamii ijayo na taifa kwa jumla.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma akiweka jiwe la Msingi Mradi wa Kituo cha Afya cha Iragua Wilayani Ulanga amesema Serikali ina nia njema na watu wake na ndio maana Mhe. Samia Suluhu Hassan anahangaika muda wote kutafuta fedha kwa ajili ya maendeleo yao.

Hata hivyo amesema nia hiyo njema inafifishwa na watendaji wa Serikali wachache na wasio waaminifu kiutendaji na kuchelewesha maendeleo ya wenzao hususan katika suala nzima la usimamiaji wa miradi ya maendeleo, hivyo amechukua fursa hiyo kuwakumbusha watendaji hao kufanya kazi kwa mujibu wa sharia, kanuni, taratibu na kwa mujibu wa taaluma zao na uzalendo.

Ukiwa Wilayani Ulanga Mwenge wa uhuru umepitia miradi sita yenye thamani ya shilingi za kitanzania ......ambayo yote imekubaliwa na Mwenge huo kuendelea na utekelezaji wake, Mwenge wa Uhuru kesho utakamilisha mbio zake Mkoani Morogoro kwa kukimbizwa katika Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero na siku ya Septemba 02 utakabidhiwa Mkoani Iringa.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.