MWENGE WA UHURU WAMULIKA MIRADI YA THAMANI YA ZAIDI YA BIL 1.5 IFAKARA MJI
Mwenge wa Uhuru umendelea kukimbizwa Mkoani Morogoro tangu ulipowasili Aprili 20, 2024 hadi leo Aprili 26, 2024 umekwisha pitia miradi ya maendeleo mbalimbali katika Halmashauri saba kati ya Halmashauri Tisa za Mkoa wa Morogoro.
Leo Aprili Aprili 26, 2024 Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya ya Kilombero Halmashauri ya Ifakara Mji na Kupitia miradi ya maendelep Nane yenye thamani ya Shilingi Bil. 1,586,216774.50.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo: nguvu za wananchi shilingi 23,600,000.00, Halmashauri shilingi 85,568700.00, Serikali Kuu 637949954.50 na wahisani au wadau wengine wa maendeleo wamechangia shilingi 839,098120.00
Moja ya miradi ya maendeleo iliyotembelewa ni Pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Mhelule kilichopo Tarafa ya Mang’ula wilayani kilombero Mkoani Morogoro wenye gharama ya shilingi 542,989,954.5 baada ya kupata fedha kutoka mfuko wa Maji wa Taifa – NWF na utanufaisha wakazi wapatao 2,838
Akiwa katika eneo hili Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava alisitiza na kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kuandaa program maalum ya kuwawezesha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) ngazi ya Wilaya ili waweze kuelewa vema mfumo wa NeST unavyofanya kazi jambo litakalowarahisishia wajumbe hao kufuatilia mfumo huo kufanya kazi inavyotakiwa na hivyo kutoa matokeo Chanya na yanayotarajiwa na Serikali.
Katika hatua nyingine Mwenge huo wa Uhuru uliona shughuli za utunzaji mazingira zinazofanyika kando ya mto Lumemo unaopita katikakati ya Mji wa Ifakara ambapo kulikuwa na kampeni ya kupanda miti takribani wiki moja na kufanikiwa kupanda miti 2000. Mwenge wa Uhuru nao ulifanikiwa kufika katika eneo hilo na kushirikiana na wananchi wa Mji wa Ifakara kupanda miti 1000 hivyo kufanya jumla ya miti iliyopandwa kufikia miti 3000.
Ujumbe wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi sio kupanda miti tu, bali kupanda miti 1,500,000 kila mwaka kama maagizo ya Serikali ambavyo yalishatolewa lakini zaidi ni kutunza miti hiyo ikue na kuleta mafanikio tarajiwa ikiwa ni Pamoja na kupunguza chanagamoto ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni Pamoja na mafuriko ambayo yamekithiri pahala pengi duniani.
Mradi mwingine uliotembelewa ni Pamoja na Uzinduzi wa Ukumbi wa Mikutano kutoka Sekta binafsi ambapo amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira mazuri ya wawekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi ili kushirikiana katika kulijenga taifa hili.
Aidha amemshukuru Mwekezaji wa Mradi huo kwa kuwa anachangia pato la Serikali kwa kulipa kodi mbalimbali za shughuli yake lakini pia kupitia uwekezaji wa mradi huo kwa vyovyote ametoa ajira kwa watanzania wenzake.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.