• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA ALIPONGEZA JESHI LA WANANCHI.

Posted on: February 4th, 2025


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amelishukuru  na kulipongeza jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia   shirika la Mzinga kwa kufanikisha zoezi la kutengeneza  kifaa saidizi (mguu bandia) chenye thamani ya shilingi milioni 2.5. Kwa ajili ya Mgonjwa aliyemuahidi kumpatia kifaa sqidizi hicho.

Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa pongezi hizo Februari 4, 2025 wakati wa tukio la kumkabidhi kifaa saidizi (mguu bandia) Bw. Jackson Mwakalinga tukio lililofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa.

Mhe. Malima amesema, kwa ushirikiano mkubwa na shirika la Mzinga wamefanikiwa kupata kifaa saidizi   kwa ndugu Jackson ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Mkoa huyo aliyoitoa Agosti 27, 2024 siku ya Maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ alipotoa ahadi ya kumpatia mgonjwa huyo kifaa saidizi cha kumsaidia kutembea.  

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kulipongeza JWTZ kwa jitihada zinazofanywa na jeshi la wananchi hasa shirika la Mzinga Mkoani Morogoro kwa kutoa  huduma nzuri kwa jamii inayowazunguka zikiwemo huduma za afya.

“…nakushukuru sana Jenerali kwani hiki ni kielelezo cha umahiri na umakini wa jeshi la wananchi wa Tanzania maana jeshi ni jeshi wakati wa vita na ni jeshi hata wakati wa Amani..” Amesema Mhe. Adam Malima

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga na Mkuu wa kikosi MAZAO, Brigedia Generali Seif Athuman Hamisi, akielezea historia ya Hospitali ya kikosi cha Mzinga amesema hospitali hiyo ilianza 1976 kama Zahanati  iliyokuwa inatoa huduma kwa maafisa wa Jeshi na hivi sasa ni hospital inayohudumia hata wananchi wa kawaida ngazi ya Wilaya kwa huduma tofauti kama vile utoaji wa huduma za vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu  wa viungo.

Naye, Bw. Jackson Mwakalinga  ambaye alikatwa mguu wake baada ya kushauriwa na madaktari ili kuokoa uhai wake amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa moyo wake wa kumpambania kupata kifaa hicho cha kumsaidia kutembea huku akilipongeza shirika la  Mzinga kwa kufanikisha upatikanaji wa kifaa hicho.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.