• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima amshukuru Rais Samia kuwakumbuka Watoto wanaoishi mazingira hatarishi.

Posted on: December 31st, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi  na kuwapa mahitaji muhimu wakati huu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Hayo yamesemwa Disemba 30, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima alipokuwa anatoa zawadi mbalimbali kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye vituo vya kulelea watoto vya Amani Center na Mission to the Homelesss Children vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Kwa sababu hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapenzi yake kwa watoto hao wanaoishi katika makao ya kulelea watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapatia zawadi za krismas na mwaka mpya 2025.

“… nimekuja hapa kwa maelekezo mahsusi ya Mhe. Dkt. Samia Suhulu Hassan amenituma na kusema nenda ukawafikie watoto vituoni kwa kadri utakavyojaaliwa nimefika lakini nitakaa na Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuona tuwafikie watoto wengi zaidi…”  Amesema Mhe. Adam Malima


Aidha, Mhe. Adam Malima amesema Ofisi yake itatoa ushirikiano wowote kwa lengo la kufanikisha kuwasaidia watoto hao kupata huduma muhimu zikiwemo huduma za afya, elimu na huduma nyingine muhimu zitakazowawezesha kuwajengea uwezo makundi hayo maalumu na kupata fursa za kushiriki kazi mbalimbali katika jamii ili kujikwamua na umaskini.

Awali, akiwa katika kituo cha Amani Centre Mhe. Adamu Malima alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Emmanuel Mkongo kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kufuatilia kwa kina ndani ya wiki moja suala la Bima ya Afya kwa watoto wote 181 wa kituo hicho ili wapate Bima hiyo ya Afya.


Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa akiwa katika kituo cha Mission to the homeless Children kilichopo kata ya Kihonda ameagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kwenda kuangalia barabara inayokwenda kituoni hapo na kuifanyia matengenezo maeneo yote korofi ili kuondoa usumbufu wanaoupata watoto wanapokwenda shuleni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mission to the Homeless children Bw. Robert Lameck ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza lengo lao la kukuza watoto hao ambapo amesema hadi sasa kituo kimewezesha kulea watoto ambao wengine wamefanikiwa kwenda kupata Elimu ya Chuo Kikuu zikiwemo shahada ya uzamili na shahada ya uzamivu huku wengine kupata kazi mbalimbali.

Msaada huo wa Mhe. Samia Suluhu Hassan wenye thamani ya shilingi Milioni mbili na laki mbili katika vituo vyote viwili umejumuisha mchele kilogram 200, unga wa ugali kilogram 200, unga wa ngano kilogram 100, sukari kilogram 100, mafuta ya kupikia lita 40, mbuzi wawili, viungo, vinywaji, mafuta ya kupaka na sabuni.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.