• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima ataka TRA kutoa elimu kwa wazalishaji kuongeza ukusanyaji kodi

Posted on: September 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoani humo kutoa elimu kwa wafanyabiashara itakayotoa matokeo chanya katika kuongeza ukusanyaji wa kodi Mkoani Morogoro.


Mhe. Adam ametoa agizo hilo Septemba 21, 2023 wakati wa kikao cha wadau wa sekta mbalimbali za uchumi wa Morogoro kilichofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kingsway Hotel uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kikiwa na lengo la kutatua changamoto za wadau hao katika kulipa kodi.

"... elimu iwe inclusive kwa ajili ya kuweza kuadress …..sasa niwaambie msiwazarau  hawa waswahili wa mtaani ndio wanaoendesha uchumi wa nchi..." amesema Mhe. Adam Kighoma Malima.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza viongozi hao kuangalia namna bora ya kukuza mitaji na uzalishaji kwa wafanyabiashara kwa kutoa elimu itakayowasaidia wafanyabiashara katika kukuza mitaji yao na sio elimu ya shule, kwani wafanyabiashara hao ndio chachu ya maendeleo katika Mkoa.

Sambamba na Hilo, Mhe. Malima amethibitisha kuwa Mkoa huo una fursa nyingi za uzalishaji mali ikiwemo mazao kama Kakao, Miwa na Karafuu, hivyo amezitaka taasisi hizo kutenga fedha kwa wazalishaji ili kuwa na walipa kodi wengi na wa uhakika.

Katika hatua nyingine, Mhe. Malima amewataka wafanyabiashara kuifanyia kazi elimu inayotolewa kwao na TRA ikiwemo elimu ya matumizi mashine ya EFD kwani baadhi ya wafanyabiashara wameonekana hawatekelezi majukumu yao  ipasavyo na kufanya ukusanyaji wa mapato serikalini kuwa ya chini.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro Bw. Chacha Gotora amesema TRA itahakikisha inaboresha utoaji wa huduma na utengenezaji wa mahusiano kati ya ofisi yao  na wadau mbalimbali wa kodi hususan  kuwatembelea na kutambua changamoto mbalimbali walizo nazo zinazohusu kodi na kuzitatua.

Nae, Mwenyekiti TCCIA Mkoani humo amewaonya wafanyabiashara kuacha tabia ya udanganyifu kwa kutumia mfumo wa kielektroniki vibaya kwa kuwatolea wanunuaji wa bidhaa risiti zisizo na majina yao pamoja na gharama tofauti za manunuzi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria huku akitoa angalizo kwa wafanya biashara hao kuwa makini katika kuangalia jina na gharama za risiti walizofanyia manunuzi.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.