• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro amshukuru Dkt. Samia kutoa bilioni 8, ataka ufaulu uongezeke.

Posted on: January 5th, 2024

Wadau mbalimbali Mkoani Morogoro wametakiwa kuongeza msukumo wa ufaulu kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari ikiwa ni alama ya shukrani na kutimiza ndoto za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za ‘Boost’ mkoani humo.

Hii ni Shule mpya ya Msingi Mgaza iliyojengwa kupitia mradi wa Boost kwa gharama ya shilingi milioni 473.

Hayo yamebainishwa Januari 4, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambapo pia alitembelea shule mbili za BOOST za Halmashauri hiyo kati ya shule 17 zilizojengwa Mkoani humo.


Muonekano wa shule mpya ya msingi ya Viwandani.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema Rais Samia ametoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya kupitia mradi wa ‘boost’ ambapo Mkoa huo umefanikiwa kujenga shule mpya 17 na kuwataka wadau Mkoani humo sasa kujielekeza katika kuongeza ufaulu wa wananfuzi kama alama ya shukrani  kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

“...kwa hiyo tuna shule za Boost 17...tukitaka kumtendea haki Dkt. Samia Suluhu Hassan tuongeze kiwango cha ufaulu cha Watoto”. Amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bw. Ally Machela amesema Halmashauri hiyo imefanya utafiti wa kubaini maeneo ya kujenga vivuko kwa ajili ya kuwarahisishia wanafunzi kufika maeneo wanayosoma wakiwa salama ikiwemo kata ya Mafisa ambapo tayari imeandika barua kuomba kupatiwa mataluma ya kujengea vivuko hivyo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Pascal Kihanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akibainisha kuwa kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani ametoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, Maji na Umeme katika Manispaa hiyo.

Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya halmashauri ya manispaa ikiwemo miradi wa Reli ya Kisasa ya umeme ya SGR, Hospitali ya Manispaa na miradi ya maji ya Mamlaka ya Maji na USafi wa Mazingira Mkoa wa Morogoro – MORUWASA.

Kwa upande wa miradi ya Elimu iliyotembelewa na kuwekewa mawe ya msingi ni Pamoja na shule mpya mbili za BOOST za Viwandani na Mgaza, ambapo imebainishwa kuwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa darasa saba mwaka 2023 Mkoani humo ni asilimia 79 ufaulu unaotakiwa kupandishwa zaidi.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.