• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro amshukuru Rais Samia kwa kuinua Kilimo, awataka wakulima kujisajiri ili kupata mbolea ya Ruzuku

Posted on: October 2nd, 2022

 RC Morogoro amshukuru Rais Samia kuinua kilimo, awataka wakulima kujisajiri.

Katika harakati za kukuza na kuinua sekta ya kilimo hapa nchini hususani ndani ya Mkoa wa Morogoro, wakulima wametakiwa kuendelea kujisajiri ili waweze kujiweka katika mazingira sahihi ya kupata mbolea ya ruzuku kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo 2023.

RC Morogoro Fatma Mwassa akimpa zawadi mshindi wa kwanza km 5 kwa upande wa wanawake mtoto Careen Charles Kajiru, (10) kutoka shule ya Msingi Benald Bendel  Mkoani Morogoro

Fatma Mwassa (Kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa Kilimo Marathon akiwemo Jakson Swebe (wa pili kulia) kutoka Shamba Dunia. kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Morogoro Gerlad Nkamia

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Abubakar Mwassa wakati wa ugawaji wa zawadi kwa washindi wa mbio za Kilimo Marathon pamoja na utoaji wa Tuzo za kilimo kwa washiriki mbalimbali tukio lililofanyika Oktoba Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa akivishwa Medali baada ya kushiriki mbio za Marathon Oktoba Mosi mwaka huu




DC Gairo Jabil Makame akivishwa medali baada ya kukimbia mbio za Marathon Km 5

DC wa Morogoro Albert Msando alishiriki pia mbio za kilimo Marathon

DC Mvomero Halima Okash akihojiwa na MC mara baada ya kukamilisha mbio za kilimo Marathon

Watendaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya morogoro na Katibu Mwenezi wa CCM Morogoro Athon Mhando (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja

Fatma Mwassa amesema kuwa zoezi la kujisajiri ndio kigezo pekee kitakachowawezesha wakulima kupata mbolea za ruzuku kwa urahisi na kama mkulima hatajisajiri hatapata mbolea hiyo kwa wakati, hivyo amewataka wakulima wote kufanya jitihada za kujisajiri.

“wakulima wengi hawajajisajiri na wasipojisajiri watapoteza fursa ya kupata ruzuku ya mbolea, na mwisho wa kujisajiri ni Disemba mwaka huu” amebainisha Fatma Mwassa.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amefafanua kuwa Mkoa wa Morogoro una zaidi ya wakulima laki nne na elfu sabini (470,000) lakini mpaka sasa waliojisajiri ni wakulima asilimia 33 pekee.

DC Ulanga Ngollo Malenya alimaliza mbio za Kilimo Marathon

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoani Morogoro Dkt. Rozaria Rwegasira alikimbia mbio hizo

Katibu Tawala Msaidizi Elimu (REO) Morogoro Germina Mng'aho alikuwepo kwenye mbio hizo

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huo amewaomba wanaMorogoro kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kudhamiria kwa dhati kuinua kilimo hapa nchini kkwa kutoa Ruzuku ya bei ya mbolea kwa takribani nusu ya bei iliyokuwa inauzwa awali, kwani amesema mfuko uliokuwa unauzwa shilingi 130,000 sasa utauzwa kwa shilingi 70,000/= pekee. Fatma Mwassa ametumia fursa hiyo kuwaagiza Maafisa Kilimo Mkoani humo na wanahabari kusaidia kutoa taarifa hiyo kwa wakulima wajisajiri ili waweze kupata mbolea hiyo ya ruzuku.

RC Fatma Mwassa (wa pili kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro  kulia, wakicheza Muziki kutoka bendi ya TOT  mara baada ya kukamilisha mbio za Kilimo Marathon

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amewakaribisha wananchi wote kwenye tukio la uzinduzi wa msimu mpya wa kilimo 2023 tukio ambalo litafanyika Oktoba 4 mwaka huu Wilayani Kilosa Mkoani humo ambapo jumla ya Ekari 5,496 zitagawanywa kwa wananchi, emaeneo wanayopewa wananchi hao yanatoka katika mashamba yaliyofutiwa umiliki na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakizungumzia kuhusu Mbio hizo za Marathon, washiriki wa mbio hizo akiwemo Abraham Mwaikwila kutoka Ulanga wamesema utaratibu wa mbio hizo kipindi msimu ujao ni vema waandaaji wakagawa washiriki kulingana na umri wao, unaolingana yaani kuwepo na kundi la wazee  na vijana ili mshindi apatikane kwa haki kwa kuwa mtindo wa sasa mfano Mzee wa miaka 55 kwa vyovyote hawezi kumshindana Kijana wa miaka 20 au 25.

Mbio za Kilimo Marathon 2022 zimefanyika katika Viwanja vya Jamhuri, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa, ambapo kivutio kikubwa kilikuwa mshindi wa kwanza km 5 kwa upande wa wanawake umenyakuliwa na mtoto wa umri wa miaka 10 Careen Charles Kajiru, anayesoma shule ya Msingi Benald Bendel  Mkoani Morogoro  ambaye amepata Medali na kufanya kuwa na jumla ya Medali 9 za mashindano mbali mbali ya mbio yakiwemo mshindano ya Selous Marathon, Kilimo Marathon pamoja na UMITASHUMTA huko Tabora.

Hilary Sagara Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro alikimbia mbio za km 5 za Kilimo Marathon

Tukutane kilimo Marathon ya mwakani 2023


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.