• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Morogoro : Tunawajibu wa kujitoa tunapohitajika na nchi yetu

Posted on: July 26th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka watanzania wote kuwa wazalendo katika kujitoa kwa ajili ya nchi kama ilivyokuwa kwa mashujaa wetu wakiwemo mashujaa wa Morogoro waliopigana vita ya mwaka 1978-1979 dhidi ya Uganda.

Mhe. Malima amesema hayo Julai 25, mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya  mashujaa waliopoteza maisha yao wakitetea, kupigania na kulinda  uhuru wa Tanzania katika mnara wa mashujaa uliopo Manispaa ya Morogoro.

"...tunachofanya ni kukumbushana sote tunawajibu wa kujua kwamba tunapohitajika na taifa letu tunawajibu wa kujitoa kwa hali na mali na hata Maisha yetu kwa ajili kutetea uhuru na Taifa letu..." amesema Mhe. Malima

Aidha, Mhe. Malima amesema mashujaa hao walipambana kwa hali na mali kwa ajili ya kuitetea nchi ya Tanzania wakiwa katika maeneo mbalimbali wakiwemo mashujaa wa Morogoro kwani amesema, walijitoa  kwa uzalendo mkubwa kwa kuweka rehani maisha yao kwa ajili ya Taifa.

Kwa sababu hiyo, Mhe. Malima  ameungana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi katika eneo la mnara wa mashujaa kuwakumbuka na kuwaombea kheri mashujaa hao ikiwa na ishara ya kujali na kudumisha misingi ya amani na utulivu katika kuendelea kuwaenzi vizazi na vizazi.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kumekuwa na misingi mizuri na imara iliyojengwa na waasisi wetu waTaifa hili wakiwemo Baba wa Taifa hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ambao wamesababisha uzalendo hapa nchini na kuishi kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake, Bw. Jackson Mzee Mkazi wa Lukobe amewasisitiza vijana kuwa na moyo wa kizalendo bila kujali malipo kama walivyojitolea mashujaa hao wanaokumbukwa hadi sasa kwani vijana ndio wenye kujenga Taifa.

Kila mwaka,Tanzania ina siku moja kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mashujaa waliopoteza Maisha yao wakiutetea, kuupigania na kulinda uhuru wa Tanzania.

Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.