• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MWASSA ATAJA MAFANIKIO YA SERIKALI SEKTA YA ELIMU

Posted on: September 9th, 2022

RC MOROGORO ATAJA MAFANIKIO YA SERIKALI SEKTA YA ELIMU, ATAKA WATOTO WA JAMII YA WAFUGAJI KUANDIKISHWA SHULE.

Serikali ya awamu ya sita katika mwaka wa fedha 2021/2022 imetumia zaidi ya shilingi Bil.38 kwenye  Sekta ya Elimu Mkoani Morogoro kuboresha miundombinu mbalimbali ya kujifunza na kujifunzia kwa lengo la kuboresha Sekta ya Elimu Mkoani humo.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Aboubakar Mwassa Septemba 9 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa vitabu vya miongozo ngazi ya Mkoa vilivyotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI vikiwa na lengo la kuboresha Elimu kwa ngazi ya Msingi na Sekondari.

Akiongea na wadau wa Elimu wa Mkoa huo wakiwemo walimu, Ukumbi wa TANZANITE katika Halmashauri ya Manispaa ya Morooro, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina budi kupongezwa  kwa kazi kubwa ya kuboresha Elimu katika Mkoa huo.

Akibainisha zaidi Fatma Mwassa amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 walimu 1800 walipandishwa madaraja huku jumla ya vyumba vya madarasa 908 vyenye thamani ya shilingi 19Bil. vimejengwa kupitia fedha za UVIKO 19.

Aidha, amesema Serikali ya awamu ya sita imejenga jumla ya shule mpya za Sekondari 13 na kugharimu jumla ya shilingi 4.7Bil. Pamoja na mabweni 4 kwa gharama ya shilingi milioni 320. Pamoja na miundombinu hiyo bado amesema Serikali hiyo imetoa shilingi 14.1Bil kwa ajili ya Elimu bila malipo kwa kipindi hicho mwaka 2021/2022 pekee.

Kwa upande wa mafunzo kwa Walimu Fatma Mwassa amesema katika kipindi hicho jumla ya walimu 1853 wamepata mafunzo kazini, mafunzo ambayo ni endelevu na kutumia fursa hiyo kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro Kumpongeza Mhe. Samia suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali yake.

Katika hatua nyingine Fatma Mwassa amesema, Elimu ni haki ya kila mtoto, kwa sababu hiyo amewaagiza Viongozi ndani ya Mkoa huo hususan walimu, kuhakikisha wanaandikisha kila mtoto pindi muda huo utakapofika huku akisisitiza watoto kutoka Jamii ya Wafugaji kutoachwa hata mmoja.

“sasa niwakumbushe tu kwamba Elimu ni haki ya kila mtoto, hata yule ambaye amezaliwa, wazazi wake hawajatilia umuhim wa Elimu sisi viongozi wa Serikali mkiwemo ninyi walimu mnawajibika kuhakikisha watoto wote wanapata Elimu, na hasa ukizingatia kuwa Elimu ni bure kuanzia Msingi Mpaka Sekondari, kwa hiyo tunavoandikisha tusiziache kando jamii za wafugaji” ameagiza Fatma Mwassa.

Pamoja na maagizo hayo amewataka Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo kutoa ushirtikiano wa kutosha katika ngazi ya shule, Kata na Wilaya kuhakikisha walimu wanafanya kazi zao ipasavyo lakini pia wanafunzi wanafundishwa vizuri na kufaulu mitihani yao na kusimamia miongozo iliyoko kwenye vitabu hivyo ili Mkoa uweze kupiga hatua mbele katika Sekta hiyo ya elimu.

Akitoa utangulizi wa kikao hicho cha wadau wa Elimu ngazi ya Mkoa, Afisa Elimu Mkoa wa Morooro Germana Mung’aho amesema, miongozo hiyo mitatu inakwenda kuleta mabadiliko makubwa sana katika sekta ya Elimu na kuwa nyezo muhimu kwa walimu katika kufanyia kazi ili kuboresha elimu ndani ya Mkoa huo.

Akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo, amesema wameyapokea maagizo yaliyotolewa na kiongozi wao bila kusita na wako timamu kuyatekeleza kwa kasi inayotegemewa na kiongozi wao.

Baadhi ya wadau wa kikao hicho hususan walimu, wao pamoja na kushukuru ujio wa miongozo hiyo bado wanashauri kuwepo jitihada zaidi za kuongeza walimu wa masomo ya Sayansi, kwa kuwa wamesema shule nyingi zina wanafunzi hadi 600 lakini mwalimu wa somo la Hisabati au fizikia ama baolojia anakuwepo mwalimu mmoja jambo ambalo wanadai ni ngumu kwa mwanafunzi kuelewa masomo hayo.

Afisa Elimu Msingi kutoka Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Witness Kimoleta amesema ili kupata matokeo mazuri kwenye mitihani, Mkoa hauna budi kuwekeza katika ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi za chini ikiwa ni pamoja na kuwa na mitihani ya mara kwa mara, kufanya Tathmini na ufuatiliaji wa kutosha.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Vigoi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani humo, katika kuboresha Elimu anashauri maeneo mawili yasimamiwe kikamilifu katika ufuatiliaji wa wanafunzi ili kupunguza utoro, lakini pia kufuatilia kwa karibu wanafunzi kupata chakula cha mchana na wazazi ambao hawatekelezi maamuzi hayo itafutwe mbinu ya kutatua changamoto hiyo.

Uzinduzi wa vitabu hivyo vya miongozo ngazi ya Taifa ulifanyika Mkoani Tabora Agosti 4 mwaka huu na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA, mojawapo ya miongozo hoyo ni “Mkakati wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi”.

Miongozo mingine ni pamoja na  “Changamoto katika uboreshaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari, nini kifanyike?” na “Mwongozo wa Uteuzi wa Viongozi wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa”.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.