Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma mwassa ameunda kamati ya watu 5 ambao watashirikiana na kamishna wa ardhi wa Wilaya ya Mvomero na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kuhakiki na kupima eneo lenye ekari 5,000 ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliagiza eneo hilo kugawanywa kwa wananchi waishio eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la msitu wa kuni wa CCT.
Mhe. Fatma Mwassa ameunda Kamati hiyo Februari 18 mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhaara na wananchi waishio eneo la msitu wa kuni wa CCT Wilayani Mvomero Mkoani Moroggoro.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameunda kamati hiyo ambayo wajumbe wake ni wananchi waishio katika eneo hilo lengo kuu la kuwashirikisha wananchi hao ni kuhakiki na kupima ekari hizo 5,000 ili kuondoa utata ambao unaweza kujitokeza baadae.
wajumbe wa kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa kwa lengo la uhakiki upimaji ardhi kwenye eneo la ekari 5,000 wakiwa wamesimama mbele ya hadhara kwa ajili ya utambulisho.
“...na sasa tuna kamati, na hii itatusaidia sana kwenye kutatua changamoto...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameiagiza TFS kwenda kung’oa mahindi yao katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya uhifadhi wa msitu huo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa eneo hilo.
Wananchi wakiwasikiliza viongozi mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la msitu wa kuni CCT Wilayani Mvomero.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka wananchi kutoa kero zao bila woga mbele ya viongozi wao pindi wanapo watembelea ili kutatua kero na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli akitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa na wananchi waliodhuria mkutano huo.
Awali, Bwana Denis Leo mkazi eneo hilo ameilalamikia TFS kwa kuwaondoa katika eneo la hifadhi na wao kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kilimo jambo ambalo tayari Mhe. Mkuu wa Mkoa amekwisha litolea maelezo na maelekezo.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.