• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC SANARE KUANZISHA MTIHANI WA ‘’MKUU WA MKOA’’

Posted on: February 20th, 2021

Baada ya Mkoa wa Morogoro kufanya vizuri katika mitihani mbalimbali huku ukishika  nafasi ya nane mwaka jana kwa matokeo ya darasa la saba kutoka nafasi ya 16 mwaka 2019, Mkoa huo sasa umekuja na mkakati wa kuongeza ufaulu wa mitihani kwa wananfunzi Mkoani humo.

Mkoa huo unatarajia kuanzisha mtihani  utakaojulikana kama “MTIHANI WA MKUU WA MKOA” unaolenga kuhamasisha ufaulu, kuwaandaa na kuwahamasisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa ufanisi zaidi na watakaofanya vizuri kupewa kupewa zawadi ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira mazuri wafikapo Chuo Kikuu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare Februari 20 mwaka huu alipotembelea  Shule ya Sekondari ya  Dakawa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo kutokana na fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

‘’Nina mpango kama Mkuu wa Mkoa, kutafuta mtihani utakaoitwa MKUU WA MKOA,  huo Mkuu wa Mkoa utakuwa unafanywa  na madarasa yale ya mitihani ya  form six, form four na form two na yataendana na zawadi na huu mtihani unafanywa ndani ya Mkoa na wale wa form six watakaopata division one we grantee them wapate mkopo waingie chuo kikuu tuhakikishe wanapata mkopo’’ amesema sanare

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Sanare akitoa zawadi kwa wanafunzi watatu wa Shule ya Sekondari ya Dakawa waliofanya vizuri katika mtihani wao wa Moko wa kidato cha sita.

Aidha, Loata sanare amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kujiepusha na mambo  ambayo yanaweza kuwakwamisha kimasomo ili waweze kutimiza ndoto zao huku akiwasisitiza kufanya vizuri mitihani yao ili kuwa miongoni mwa shule 10 bora zitakazofanya vizuri katika mitihani ijayo.

Wakizungumzia changamoto zilizopo shuleni hapo, wanafunzi wa shule hiyo akiwemo Octavina Steven ambaye pia ni Dada Mkuu wa shule hiyo ameiomba Serikali kuwajengea uzio kuzunguka shule hiyo hususan mabwenini ili kuwa na uhakika na ulinzi kwao na mali zao .

Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dakawa, wa kwanza kushoto ni Dada Mkuu wa shule hiyo Octavina Steven na viongozi wengine.

Naye Salah Justine wa kidato cha sita anayechukua mchepuo wa HKL amesema wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vitabu na kuomba wasaidiwe vitabu ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Naye Noela Christopha mwanafunzi wa kidato cha sita HGK  amesema shule hiyo ina ukosefu wa Nesi  hali inayopelekea akitokea mgonjwa kushindwa kumuhudumia kwa wakati.

Akizungumza na wanafunzi hao Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Albinus Mgonya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero amewasisitiza wanafunzi hao kutekeleza maagizo aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ikiwa ni pamoja na kutii maelekezo halali ya walimu wao na kuzingatia masomo.

Shule ya Sekondari ya Dakawa ilianzishwa mwaka mwaka 1992 ikiwa ni Shule mchanganyiko (wavulana na wasichna) mwaka 2006 Shule hiyo ilibadilishwa kuwa  Shule ya wasichana ikiwa na michepuo ya HGK, HGL, HGE na HKL.

Shule hiyo hadi sasa ina wanafunzi  422 ambapo kidato cha tano ni wanafunzi 209  na kidato cha sita 213, ina walimu 31 na watumishi wasio walimu 3.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.