• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Shigela akasirishwa na Daktari aliyemsababishia mama kujifungulia ndani ya Bajaji, amsweka ndani.

Posted on: July 28th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ameamuru kukamatwa kwa Daktari Cassius Lwebangira wa Kituo cha Afya cha Mikumi kwa tuhuma ya  kumchelewesha mama mja mzito na kusababisha mama huyo kujifungua akiwa ndani ya Bajaji kwa sababu ya kutaka fedha.

Martine Shigela ametoa agizo hilo Julai 27 mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhara  uliofanyika katika mji mdogo wa Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani humo ambapo ameendelea kupokea kero za wananchi wa Wilaya hiyo na kuzitatua.

Awali kijana aliyejulikana kwa jina la Abdallah Agustino mkazi wa Mikumi akitoa kero yake Mbele ya Mkuu wa Mkoa alimueleza kuwa mnamo mwezi Aprili mwaka huu alimpeleka mke wake Jenifa Francis katika Kituo cha Afya cha Mikumi akiwa ni mja mzito ili kupata huduma ya kujifungua katika kituo hicho.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah Daktari aliyekuwepo zamu Cassius  Lwebangira alimueleza Abdallah kuwa mke wake anatakiwa afanyiwe upasuaji na kumtaka ampe fedha  kiasi cha shilingi laki moja na ishirini ili atumie vifaa vyake katika upasuaji huo badala ya kwenda kuvinunua sehemu nyngine.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abdallah anasema baada ya kushindwa kutoa kiasi hicho cha fedha alimwambia Abdallah achague mawili au kumpe kiasi cha fedha hizo ama kuondoka na mke wake hospitalini hapo huku mama huyo akiwa anahangaika  uchungu wa uzazi hali iliyomfanya baada ya muda kujifungua akiwa ndani ya  Bajaji njiani  wakielekea Kituo Cha Afya cha St. Kizito cha Mikumi.

Akijibu swali la Mkuu wa Mkoa juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Daktari huyo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa George Kasibante alimweleza Mkuu wa Mkoa tayari hatua zilishachukuliwa ikiwa ni pamoja na kubadilisha uongozi wa Kituo hicho cha Afya pamoja na kumpa Onyo mhusika.

Hata hivyo  Mhe. Shigela hakuridhika na hatua zilizochukuliwa dhidi ya Daktari huyo ukilinganisha na ukubwa wa kosa alilolifanya na kulazimika kuagiza akamatwe na polisi ili alale rumande huku akimuagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Manyama Tungaraza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa kina huku akiagiza akidhibitika na kosa aweze kuchukuliwa hatua nyingine za kinidhamu.

Aidha, Mhe. Shigile ametumia fursa hiyo kuwataka watumishi wengine wa Umma wa Sekta ya Afya Mkoani humo, kuacha mara moja kuwanyanyasa akina mama hasa waja wazito na kwamba jambo hilo halikubaliki  kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha Afya za wananchi wake.

Mkuu wa Mkoa Martine Shigela yuko kwenye ziara ya kutembelea miradi itakayopitiwa na mwenge wa uhuru 2021. Hadi sasa tayari amefanya ziara hiyo katika Wilaya za Gairo, Kilosa na leo yuko Wilaya ya Morogoro.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.