• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Shigela ataka Watendaji kujipanga ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Posted on: August 21st, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewataka Wakurugenzi Watendaji na Madiwani wa Halmashauri zote Mkoani humo kuwa na utaratibu wa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wananfunzi wa kidato cha kwanza kila ifikapo mwezi Julai ili kuondokana na mazoea ya kukimbizana na ujenzi huo inapofika mwezi Desemba kila mwaka.

Martine Shigela ametoa maagizo hayo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kupokelewa mwezi Januari 2022 kilichofanyika katika ukumbi wa CCT uliopo Kilakala katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.


Amesema, viongozi wote wanajua changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na miundombinu mingine ambayo hujitokeza kila mwaka lakini bado viongozi hao husubiri maelekezo ya viongozi wa Serikali kutoka juu na ikifika mwezi Disemba kuanza kukimbizana kwa ajili ya kutekeleza maagizo hayo kama vile hawajua uwepo wa changamoto hiyo.

Kwa sababu hiyo, Martine Shigela ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, amezitaka Halmashauri za Mkoa huo kujipanga katika kukabiliana na upungufu wa madarasa kila ifikapo Mwezi Julai ili ifikapo mwezi Disemba changamoto hiyo iwe imetatuliwa.

‘’.. Kwa nini hatujipangi kuanzia Julai tukaanza kujenga kidogo kidogo kwa nguvu za wananchi na Halmashauri yenyewe, sasa hivi tupo mwezi wa nane tunaingia wa tisa, tuna miezi mitatu ya kujipanga vizuri ili matokeo yakitoka jambo hili liwe limekamilika..” alisisitiza Mhe. Shigela.

Naye Katibu Tawala Msaidizi upande wa Mipango na Uratibu Anza Amen Ndossa amesema, kutokana na upungufu wa madarasa 428, Mkoa unalazimika kuanza mapema kuunganisha nguvu na kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa Elimu kujenga vyumba hivyo 428 vya madarasakwa shule za Sekondari kabla ya mwezi Disemba, 2021.


‘’Tusipojipanga mapema baadhi ya wanafunzi watashindwa kujiunga na Kidato cha kwanza kwa kukosa vyumba vya Madarasa’’ Amesema Ndossa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wajumbe wa kikao hicho wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri  na baadhi ya Madiwani pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri, licha ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa kuja na utaratibu wa kuanza maandalizi ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa mapema, wamemuahidi kutekeleza maagizo hayo aliyoyatoa ili kuondokana na changamoto hiyo.

Kwa mujibi wa Katibu Tawala Msaidizi Anza Amen Ndossa, Mkoa wa Morogoro  unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 428 kwa ajili ya wanafunzi 21,400 wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kupokelewa mapema mwezi Januari 2022.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.