• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Serikali yaagiza kuajiri maafisa utamaduni.

Posted on: August 16th, 2023

Serikali imeagiza Mikoa na Halmashauri nchini kuajiri maafisa  utamaduni na Maafisa michezo wa muda katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri ili kusaidia kutekeleza majukumu ya kada hizo na kukuza sekta ya utamaduni, Sanaa na michezo katika maeneo yao.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha viongozi na wakuu wa taasisi kutoka Wizara hiyo.

Agizo hilo limetolewa Agosti 16 mwaka huu na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana (Mb) wakati akifungua kikao kazi kilichohusisha viongozi wa Wizara hiyo na wakuu wa Taasisi za sanaa na Utamaduni hapa nchini kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Magadu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Waziri Dkt. Pindi Chana amebainisha kuwa kati ya halmashauri zaidi ya 180 zilizopo hapa nchini zipo ambazo hazina Maafisa utamaduni na michezo hivyo ameitaka Mikoa na Halmashauri ambazo hazina Maafisa hao kutoa ajira ya muda kwa watumishi wa kada hizo kutokana na umuhimu wa michezo na utamaduni ili kuongeza kasi ya utendaji kazi katika maeneo yao.

“...nimeshatoa maagizo, tuone namna gani katika kipindi hiki cha mpito tunaposubiri vibari vya kuwaajiri rasmi, lazima tuwe na watu wanao kaimu nafasi hizo ili shughuli ziende...lazima Halmashauri, lazima Mikoa iweke mtu anaye kaimu ili kazi ziende...” amesema Dkt. Pindi Chana.

Aidha, Waziri huyo amesema kila Mkoa na Wilaya kuna kamati za michezo ambazo wenyeviti wake ni Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya ambao wanafanya nao kazi ili kuhakikisha kuwa maelekezo yanayotolewa yanafanyiwa kazi kuanzaia ngazi ya chini.

Pamoja na Maagizo hayo Waziri Pindi Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi katika sekta ya afya, maji, umeme hata kwenye sekta ya michezo ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya michezo pamoja na kujenga mahusiano mazuri ya kiutamaduni na mataifa mengine.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma (Mb) amezitaka taasisi zinazohusika na masuala ya michezo, utamaduni na sanaa kufanya kazi kwa ushirikiano,na kuwataka washiriki kupitia kikao hicho kuweka maazimio ya pamoja ili kuendelea kukuza sekta ya Utamaduni, sanaa na michezo hapa nchini.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma akizungumza wakati wa kikao kazi cha viongozi na wakuu wa taasisi kutoka Wizara hiyo ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akitoa salamu za Mkoa ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa kikao hicho ambacho kina manufaa katika kukuza sekta ya utamaduni na michezo pamoja na pongezi hizo ameiomba Wizara hiyo kuongeza jitihada zaidi kutoa elimu kwa watanzania kujitambua, kuthamini na kujivunia utamaduni wao.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakati wa kikao kazi cha Wizara hiyo.

Kikao kazi hicho kimelenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Wizara hiyo ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na wakuu wa Taasisi zinazofanya kazi sambamba na Wizara hiyo zikiwemo Baraza la Taifa la Sanaa, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania na nyingine zilizoalikwa kwenye kikao hicho.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya kikao kazi cha Wizara hiyo.

Huyu ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na uzalishaji Dkt. Rozalia Rwegasira akiwa kwenye kikao kazi cha Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akitoa salamu za Wizara hiyo wakati wa kikao.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Rebeca Nsemwa akitoa salamu za Wilaya ya Morogoro wakati wa kikao kazi cha Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo.

MWISHO.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.