• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI MAPATO SASA KIDIJITALI

Posted on: February 11th, 2022

MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI MAPATO YA MAEGESHO YA VYOMBO VYA MOTO KUANZA KUKUSANYWA KIDIJITALI.

Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya moto vya usafiri wa nchi kavu Mkoani Morogoro utaanza kukusanywa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kuanzia Machi Mosi mwaka huu, imefahamika.

Taarifa hiyo imetolewa Februari 9, mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Martine Shigela wakati anaongea na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mfumo mpya wa ukusanyaji ushuru wa maegesho ya vyombo vya moto Mkoani Morogoro

Albert Msando Amesema makusanyo hayo kwa Sasa yatafanyika kwa kutumia mfumo wa kielektroniki uitwao TerMIS ambapo malipo yote yatafanyika kwa kutumia control namber mfumo ambao Mkoa wa Morogoro ulikuwa haujaanza kuutumia na Sasa unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Machi 1, mwaka huu, ameeleza  Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha, Mhe. Albert Msando akiongea na waandishi wa habari amebainisha lengo Kuu la mabadiliko hayo kuwa ni pamoja kuongeza mapato ya Serikali, kuepusha matumizi ya fedha mbichi na kuondokana na Kero zilizokuwa zinajitokeza siku za nyuma za kufukuzana na wateja wao.

Kwa sababu hiyo, Mkuu wa Wilaya amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto kufuata utaratibu huo mpya ulioanzishwa na Serikali kupitia Wakala wa Barabara wa Mjini na Vijijini - TARURA wa kulipa ushuru kwa hiari, kwani fedha zinazoparikana zinalenga kusaidia Maendeleo ya wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Naye Mkuu wa Kitengo Cha TEHAMA - TARURA Stanley Mlula amesema serikali inahitaji watu kuelewa  vema lengo la kutumi contorl number ya GepG ili kuunganisha na namba za vyombo vya usafiri na kuweza kutoa ankara ambayo italipa moja kwa moja kupitia simu au benki ili kurahisisha utendaji kazi katika maeneo yote hapa nchini.

 Sambamba na hayo, Mkuu wa Kitengo Cha Sheria - TARURA Shaban Mdagano ameeleza umuhim wa wananchi kuzijua baadhi ya kanuni zinazoendana na mfumo huo ili waweze kutekeleza kwa ufanisi zaidi kanuni hizo.

Mkuu wa Kitengo Cha Sheria - TARURA Shaban Mdagano

Baadhi ya kanuni zinazotakiwa kujulikana ni pamoja na Mteja anayeshindwa/anayekataa kulipa USHURU wa maegesho wakati wa kuegesha gari au chombo chake cha moto baada ya Siku Kumi na Nne atatozwa faini ya shilingi elfu kumi pamoja na fedha  ulizotakiwa kulipa.

Endapo mteja atashisdwa kulipa tena faini hiyo atafikishwa Mahakamani ambako huko ikithibitika ana kosa mteja atalazimika kulipa faini ya shilingi laki tatu au kifungo cha miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja.

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja akifungua semina hiyo ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na na baadhi ya Viongozi wa Mkoa huu, amesema Mkoa wa Morogoro unaingia katika mfumo wa kukusanya ushuru wa maegesho wa kielektroniki, mfumo huo utaondoa upotevu wa mapato yaliyokuwa hayakusanywi ipasavyo kwani kila mteja atalipa ushuru wa chombo chake anachomiliki kwa kutumia control number.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja

Hadi sasa Mfumo huu unatumika katika mikoa mitano hapa Nchini mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Mwanza, Singida, Shinyanga, Dodoma na Dar es salaam.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Zaidi ya Mil. 125 zachangwa kupitia chakula cha hisani kukarabati Hospitali ya Rufaa Morogoro.

    May 18, 2025
  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.