• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wadau wa TASAF waridhishwa na maendeleo ya wanufaika

Posted on: January 28th, 2025

Wadau wa maendeleo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) wameridhishwa na maendeleo wanayoyapata walengwa wa mradi huo ikiwa ni pamoja wengi wao kuanza kujitegemea na kuanzisha shughuli zao binafsi za kujiingizia kipato kupitia fedha za TASAF.

Hayo yamebainishwa Januari 28, Mwaka huu na Afisa Usimamizi wa Miradi ya TASAF kutoka Ubalozi wa Uswis hapa nchini Bi. Clara Minja wakati wa ziara ya kukagua miradi ya TASAF Wilayani Kilosa ili kubaini maendeleo ya miradi hiyo, changamoto pamoja na kukusanya maoni ya kuboresha zaidi uendeshaji wa programu hiyo.


Akifafanua zaidi kwa niaba ya mabalozi wengine wanaosaidia Mradi huo Bi. Clara amesema walengwa wa mradi wa TASAF wamefaidika na mradi huo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi zikiwemo Kilimo, ufugaji na biashara nyingine hivyo amesema TASAF inatoa mchango mkubwa hapa nchini katika kusaidia wananchi wanyonge kuweza kujitegemea.


"... nimefurahishwa kuona walengwa wakinionesha namna walivyofaidika na huu mradi wa TASAF ambapo wamefanikiwa kufanya shughuli za kilimo, ufugaji na biashara ndogo ndogo..." amesema Afisa usimamizi huyo.


Hata hivyo, Balozi huyo wa Uswis amesema walengwa wengi wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo na ufugaji ambapo hali ya mabadiliko ya tabia imekuwa ikiwaathiri hivyo amesema amezipokea changamoto hizo zikiwemo za kimitandao na  miundombinu na kuahidi kwenda kuzifanyia maboresho haraka.


Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Miradi ya TASAF Taifa Bw. John Steven amesema ziara hiyo ina malengo mahsusi ya kufuatilia utekelezaji wa miradi ziara ambazo hufanyika kila baada ya miezi sita ili kujua changamoto, mafanikio na kuwasikiliza walengwa katika kuboresha utekelezaji wa mradi huo.


Kwa upande wao wanufaika wa TASAF akiwemo Bw. Festo Elias ameishukuru Serikali kwa kuanzisha mradi wa TASAF na kubainisha kuwa umemsaidia kwa kiasi kikubwa hadi sasa anamiliki shamba la ekari kumi, kondoo 14 na fedha hizo zimemsaidia kujenga nyumba yake binafsi.


Naye, Bi. Jenirosa Ngangaa Mnufaika wa TASAF kutoka kijiji cha Peapea Wilayani Kilosa  ameishukuru serikali kwa kuanzisha mradi wa TASAF uliomsaidia kujikimu na kumsomesha mtoto wake kuhitimu Chuo kikuu cha Ardhi kilichopo Jijini Dar es Salaam.


Ubalozi wa Uswis ulianza kutekeleza mradi huo wa kunusuru kaya masikini Mwaka 2020 ambapo hutolewa katika vipindi viwili vya uchangiaji kwani mpaka sasa imeshachangia kiasi cha Tsh. Bil. 80 ukiwa na lengo la kushirikiana na Serikali ya Tanzania na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo nchi za Ireland, Norway na nyingine.


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.