• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wakazi Morogoro watakiwa kujitokeza kwenye mashindano ya michezo ya Majeshi.

Posted on: September 5th, 2024

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro na maeneo jirani wametakiwa kujitokeza na kuona Michezo ya Majeshi Tanzania  inayoanza kutimua vumbi Septemba 6 hadi 15,  2024, katika viwanja mbalinbali vilivyoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Wito huo umetolewa leo Septemba 5, 2024 na Mwenyekiti wa BAMMATA Brigedia Jeneral Saidi Hamisi  Saidi wakati akiongea na waandishi wa habari kutoa taarifa rasmi ya mashindano hayo kufanyika Mkoani Morogoro.

 Aidha, Brigedia Jenerali Saidi Hamisi Saidi amebainisha kuwa mgeni rasmi atakayezindua mashindano ya michezo hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambaye tayari amekwisha wasili Mkoani Morogoro.

Akifafanua zaidi, Brigedia Janeral Saidi amesema mashindano hayo yanashirikisha na kuyakutanisha majeshi ya kanda saba ambazo ni Ngome, (JWTZ) Magereza, Uhamiaji, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Zimamoto na Uokoaji, Polisi,  pamoja na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akitoa wito kwa wananchi Kiongozi huyo amesema mashindano hayo hayatahusisha kiingilio chochote katika viwanja vya michezo vilivyoandaliwa ambapo ni viwanja vya Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), viwanja Umwema JKT, na viwanja vya Jamhuri, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuangalia na kufurahia burudani za michezo ya majeahi yao ambayo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, mchezo wa masumbwi, mpira wa wavu, mpira wa mikono, kurusha mkuki, kulenga shabaha, riadha na mchezo wa vishale.

"... Nichukue fursa hii niwakaribishe wananchi katika viwanja vyote tulivyo vitangaza isipokuwa kiwanja maalum kwa mchezo wa shabaha, viwanja vingine wananchi wanakaribishwa kwa wingi kabisa ili kuja kuona burudani mbalimbali.." amesisitiza Brigedia Jeneral Saidi.

Akieleza matarajio yake, Brigedia Jeneral Saidi amesema, baada ya kumalizika mashindano hayo anaamini watakuwa na timu bora itakayoweza kushiriki mashindano mbalimbali, lakini pia watakuwa wameboresha Afya za washiriki, kuimarisha umoja na mshikamano baina ya majeshi katika utendaji kazi wao.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.