• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAKURUGENZI WAPEWA AGIZO

Posted on: August 1st, 2022

Wakurugenzi watakiwa kuandaa mashamba darasa

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mikoa inayounda Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki wametakiwa kuandaa mashamba darasa ya vipando katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi ambao hawakushiriki maonesho hayo kujifunza kilimo cha kisasa kupitia vipando hivyo ili kilimo hicho kiwaletee mazao mengi na yenye tija.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo (kushoto) akipata maelezo kutola kwa mtaalamu katika banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro

Witoa huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo Mkoani Morogoro akiwa mgeni rasmi wa siku ya kwanza ya maonesho hayo ya wakulima na wafugaji maarufu kama Nanenane Kanda ya Mashariki inayoundwa na Mikoa minne ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Wenyeji Morogoro.

Ndugu Lingo amesema, kumekuwa na dhana kwa halmashauri nyingi kuandaa vipando kwenye mabanda yao kwa lengo la kufundishia na mashindano, lakini hawaweki mikakati ya kuandaa vipando hivyo kwenye halmashauri zao ili kutoa fursa ya kutoa elimu hiyo kwa wananchi waliokosa kushiriki maeneo ya Nanenane.

Kwa sababu hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya ya Pangani ametumia maonesho hayo kuwaagiza wakurugenzi wote wa kutoka mikoa hiyo kwenda kuandaa vipando hivyo mara watakaporejea katika maeneo yao kwa lengo la kupeleka elimu hiyo kwa wananchi waliobaki huko.

“Ni kweli Halmashauri nyingi wanaviandaa vipando kama sehemu ya kufundishia na mashaindano, lakini wanaporudi kwenye Halmashauri zao  hawana maandalizi ya mkulima aliyekosa kujifunza kule kwenye nanenane ajifunze kwenye halmashauri zao” amesema.

“ ...nichukue nafasi hii kuwaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote wakirudi, waandae mashamba darasa ambayo yatawafanya wananchi waliokosa kujifunza kwenye nanenane wakajifunzie kule waliko” amesisitiza Bw. Lingo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya ya Pangani amewataka wananchi wa kutoka Mikoa hiyo na watanzania wote kwa jumla kuacha matumizi ya kilimo cha jembe la mkono, badala yake wajikite kwenye kilimo cha kutumia zana za kisasa kama matrekta ili kujipatia mazao bora na yenye tija.

Nao washiriki wa maonesho hayo akiwemo mfugaji wa ngo’ombe wa maziwa  Lina Joseph Kinabo kutoka kibaha Mkoani Pwani ameelezea ufugaji wa kisasa wa ng’ombe kwa kutumia vifaa vya kisasa kama GPS ambapo hukitumia kutambua maendeleo ya mifugo wake kwa kutumia simu ya mkononi hata anapokuwa mbali na mifugo wake.

Kaulimbiu ya maonesho ya wakulima na wafugaji (nanenane) 2022 ni: Ajenda ya 10/30, Kilimo ni Biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango Bora ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.