• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wananchi watakiwa kutunza miundombinu ya barabara.

Posted on: March 11th, 2024

Wananchi wilayani kilosa na manispaa ya morogoro mkoani humo, wametakiwa kutunza miundombinu ya barabara inayojengwa na Serikali ikiwa ni pamoja na vyuma vya madaraja ili miundombinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu kwa faida yao na vizazi vijavyo.

Wito huo umetolewa Machi 10, 2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo ya kutembelea Miradi ya maendeleo ya sekta ya miundombinu hususan barabara zinazojengwa katika Wilaya hizo.

Dkt. Mussa Ali Mussa ambaye amemwakilisha mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  ya Mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima amesema, serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo lakini kuna watu wachache ambao wanarudisha nyuma azma ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuwataka kwa umoja wao kuwa walinzi wa miundombinu hiyo.

Akiwa katika daraja la Berega Wilayani Kilosa Dkt. Mussa amewataka wananchi wanaoishi Berega na vijiji jirani na daraja hilo ambalo linaunganisha mikoa miwili ya Morogoro na Tanga kuungana na kupanda miti pembezoni mwa mto wa daraja hilo kwa ajili ya kuimarisha daraja hilo ikiwa ni pamoja na kupanda mikarafuu ambayo pia ni faida kwao.

Katika ziara hiyo, Wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Katibu Tawala huyo walitembelea miradi ya barabara ya Mfungua kinywa na Kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, daraja la mto Berega, Daraja la Mazinyungu Ilonga barabara ya Rudewa - Kilosa na daraja la Ruaha Mkuu na daraja la Ruhembe barabara ya Mikumi - Ifakara Wilayani Kilosa.

Wajumbe hao wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaendelea na ziara yao katika Wilaya ya Kilombero kwa lengo la kutembelea barabara ya Kibaoni Ifakara, ujenzi wa daraja la Chiwachiwa na ujenzi wa barabara ya Ifakara Mbingu.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.