• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI MOROGORO WATAKIWA KUZUIA HOJA ZA UKAGUZI.

Posted on: June 22nd, 2024


Watendaji wa Halmashauri Mkoani Morogoro wametakiwa kuwa mahiri katika kuzuia hoja za Ukaguzi kutojitokeza katika Halmashauri zao badala ya kuwa mahiri katika kujibu hoja hizo wakati zimejitokeza na hivyo kuiletea doa Halmashauri wanazofanyia kazi.


Ushauri huo umetolewa Juni 21, 2024 na  Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Morogoro Bw. Baraka Mfugale wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya  Malinyi Mkoani Morogoro.


Bwana Mfugale amesema, watumishi wengi wa Halmashauri wanakuwa mahiri katika kujibu hoja kuliko kuzuia ambapo amewataka kujitahidi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, Taratibu  na Kanuni (STK) zilizopo hivyo kutoa ruhusu hoja lakini pia kutoa ushirikiano wakati wa ukaguzi unapofanyika kwa lengo la kupata majibu sahihi kabla ya vikao kufanyika.


"... Ni muhimu tukapata ushirikiano mzuri wakati wa ukaguzi kuliko ushirikiano mkubwa mnaouhitaji wakati wa kikao..." amesisitiza Mfugale


kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano kwa lengo la kuendeleza Halmashauri hiyo, na kwa kufanya hivyo ni rahisi kuzuia hoja za ukaguzi.


Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa maendeleo ya Wilaya hiyo watumishi wa Serikali wanapaswa kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuepusha migongano baina yao na kuwa na malengo ya pamoja katika kufikia mafanikio ya maendeleo ya wananchi wa Malinyi.


"..Team work ndani ya Halmashauri ya Wilaya Malinyi ni mbaya sana.." Amebainisha Mhe. Adam Malima.


Aidha Mhe. Malima ameishukuru Serikali inayoongozwa na  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha matengenezo ya dharura ya barabara ya Malinyi, kuleta chakula kwa wananchi wa Malinyi walioathirika na mafuriko, lakini pia kwa kuto shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Ifakara ambapo kitapunguza adha ya umeme Wilayani humo.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi  Bw. Pius Mwelase amemtaka Mkukurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi. Rose Manumba kuwasimamia watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa kujituma kwa lengo la kuiletea maendeleo halmashauri hiyo na wananchi wake kwa ujumla.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.